Tuesday, February 12, 2013

Tazama mazoezi ya timu leo asubuhi. Mwalimu anasema vijana wapo tayari kwa kutwaa point tatu muhimu kutoka kwa vibonde Kagera Sugar.

 Suleiman Kassim 'Selembe' akiingia uwanja wa Kaitaba Bukoba leo asubuhi kujifua na timu.

 Jana Sudi alimchana mwenzie Rajabu domo kwa mpira. Angalia alivyovimba maskini, ukimwambia aseme Pepsi anasema pepthiiii maskini wee domo noma.

 Mwalimu Morroco na Mwenyekiti wakiangalia vijana wakijifua..

 Gabriel Barbosa jana alikuwa akiumwa, kila akiulizwa analia anasema anataka akapimwe Malaria. Dr akamwambia huumwi ni uchovu tu akaambiwa siku ya jana alale tuu. Leo ameamka fiti na atapiga boli kama kawa.

 Mwalimu akiangalia wachezaji wakisprint, anasema hii inawasaidia kuondoa baridi na kuongeza nguvu za miguu.

 Morroco akisisitiza jambo kwa wachezaji, hawapo pichani.

 Jerry Santo akiongoza wenzie kufanya mazoezi ya kukaa na mpira muda mrefu au wakoloni wanaita ball contol. Mh jamani leo haponi mtu, vijana wana njaa ya ushindi balaa. Halafu naskia Binslum keshaweka mambo ubaoni. Mwachemwache hiyo... eeenhhhhh jogoo hana mtoto...

                                                                   Maaambooo hayoo...       
        
 Aurora ngado kwa ngado na wachezaji hataki mchezo.

                                           Sippi akinyoosha viungo wakati wa mazoezi.


No comments:

Post a Comment