Gabriel Barbosa anasema yupo fit kwa game hatowaangusha vijana wa Tanga.
Ndugu zangu,
Timu ya Coastal union kama
ilivyoelezwa jana iliingia mjini Bukoba majira ya saa kumi na mbili kasoro
jioni ikitokea mjini Mwanza kwa usafiri binafsi. Mwanza kulikuwa na hali ya
joto na baridi ya wastani, lakini Bukoba kuna baridi na mvua kidogo.
Leo asubuhi timu ilifanya mazoezi katika uwanja wa Kaitaba
pembezoni mwa ziwa Victoria.
Hali ya hewa ni baridi na mvua, timu imefanya mazoezi katika mvua kali.
Hii itasaidia kuwaweka imara kwa maana watazoea hali hii
hata kesho wakati wa mechi kama kutanyesha
mvua hawataona ajabu wala kuhisi tofauti.
Kitu tulichokutana nacho Bukoba ni mpira wa redioni, au kule
kwetu tumezoea kuita mpira wa midomoni. Viongozi wa Kagera wanajitahidi sana kututisha ili mechi
tuione ngumu, hatujafanyiwa hujuma zozote mpaka sasa wala roho mbaya lakini
wanatumia redio zao kutoa vitisho.
Kwanza wanasema timu ya
Kagera sugar imeunda kamati ya saidia Kagera Sugar ishinde, yaani iwe ni mbiu
ya mkoa mzima wa Kagera kuhakikisha wanashinda mechi zote za nyumbani na
ugenini.
Wanasema watahakikisha uwanja unajaa mashabiki wao ili
washangilie kwa nguvu kuwapoteza malengo wachezaji wa wagosi wa kaya.
Hata hivyo blog hii ilizungumza na baadhi ya wenyeji ambao
wamesema Kagera sugar haina wapenzi hapa Bukoba, haipendwi na wala hakuna mtu
anaejishughulisha.
Malalamiko makubwa wanayoyatoa wenyeji wa Bukoba ni namna
kiwanda cha sukari cha Kagera kilivyopandisha bei ya sukari katika mkoa huu ili
pesa zinazopatikana zisaidie timu wanalipinga sana
suala hilo.
Aidha viongozi wa Kagera Sugar wanaifananisha Coastal Union
na JKT Mgambo, ati kwasababu waliwafunga mechi iliyopita tarehe 9 feb, lakini
nawasikitikia sana
kwa kufananisha mbingu na ardhi.
Kocha mkuu wa Coastal Union Hemed Morroco anasema “Sisi
tumekuja kutafuta ushindi maneno yao
hayatutishi, wachezaji wangu ni bora mara sabini ya wao, hivyo ninachotaka
kukwambia usitishike na maneno yao.”
Nae mwyekiti wa timu Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema hawezi kupoteza muda na pesa
kutoka Tanga kuja Bukoba halafu warudi bila ushindi, hicho kitu hakiwezekani
katu.
Coastal Union Wagosi wa kaya kesho watashuka dimbani katika
uwanja wa Kaitaba Bukoba kumenyana na Kagera sugar katika mchezo wao wa nne
kwenye ligi kuu Tanzania
bara mzunguko wa pili.
Kagera sugar inashuka dimbani ikiwa na point 24 katika nafasi
ya sita kwenye msimamo wa ligi wenye timu 14, wakati wagosi wa kaya wana point
27 katika nafasi ya nne. Wakishinda mchezo wa leo watakwea nafasi moja juu na
kuwa nafasi ya tatu kitu wanachokililia kwa muda mrefu.
Mungu isaidie Coastal Union Mungu usaidie mkoa wa Tanga urudishe
heshima yake ya soka iliyokuwa nayo kwa miaka mingi hata kabla ya uhuru
kupatikana mwaka 1962.
COASTAL UNION
12,02,2013
Kagera,Tanzania
No comments:
Post a Comment