Sunday, February 10, 2013

Kitu ambacho mtu yeyote hakukijua kuhusu mechi ya jana hata mwenyekiti wa timu pia alikuwa hajui, ni hiki hapa.....

 Kumbe Shaaban Kado jana alibakia dakika chache afariki dunia akiwa uwanjani. Maneno hayo alinambia Daktari wa timu wakati tunakunywa chai asubuhi hii. hakutaka kumwambia mtu kwasababu watu wangechanganyikiwa.

Angalia mchezajai wa Toto alivyochanganyikiwa, pia muangalie mchezaji wa Coastal Othman Tamim alivyochanganyikiwa, refa yeye hakuwa akijua kinachoendelea bali alikuwa akimwambia Dr vp ataamka?

 Philp Mugenzi baada ya kuiona hali ya kipa wake machozi yakaanza kumlengalenga hakutaka hata kuangalia, Selembe akawa anamuita Kado, Kado kimyaaa.... Refa akataka kuita watu, Dr akamwambia ukiita watu huyu hataamka maana watajazana na atakosa hewa wacha nimpe huduma ya kwanza nipoze mishipa ya shingo.

 Hatimae akaamka baada ya kumuinua miguu ili damu iende kwenye Ubongo, Dr alinipa ujanja huo akanambia hata marehemu Kanumba angepewa huduma ya kwanza asingeaga dunia. Maana alipojigonga kwenye mshipa wa kupeleka damu kwenye ubongo hakukuwa na mtu wa kumuinua kichwa chini mguu juu ili damu nyingi iende kichwani. Na Kado laiti asingewahiwa leo tungekuwa na msiba.

 Hapa ameamka lakini bado hali yake haikuwa nzuri, Dr alinambia Kado alipotaka kuamka alitaka kukimbia, lakini akamzuia kwani bado alikuwa akiona maruweruwe mpaka alipotulia kama dakika kadhaa.

 Baadae akaamka akapiga mpira kwa nguvu zote utadhani sie yeye aliechungulia kaburi.




Huyu jamaa wa  Toto Africa anaitwa Muddy, inasemekana aliwahi kuichezea Coastal Union, ndie aliemuumiza shaaban Kado mpaka akachungulia kaburi, inaonekana baada ya mpira kuisha alimfata Kado kumuomba radhi na baada ya hapo akamfuata beki wa Coastal Othman Tamim kumuomba radhi, maana Tamim aliumia sana kuona kipa wake alitaka kuuliwa mbele ya macho yake. Ila Muddy alifanya kitendo cha kiungwana sana kuomba radhi, natumai Tamim alimsamehe.

No comments:

Post a Comment