Saturday, February 9, 2013

Mpira ulipofika kipindi cha pili mambo yalikuwa moto lakini hatukuambulia chochote zaidi ya wachezaji wetu wanne kupewa kadi za njano....

 Selembe leo alicheza mpira wote aliofundishwa na mwalimu lakini bahati haikuwa yake.

 Shaaban Kado uzoefu ndiyo uliomsaidia kuna kipindi tulishambuliwa kwa nguvu akawa anajilaza na kumpa muda mwalimu na Captain kupanga timu upya. Safi sana Kado.

                   Hapa Messi, Barbosa na Hamad wakipasha ilikuwa dakika ya sabini ya mchezo.
                     
 Barbosa alijionyesha uwezo wake aliojaaliwa na Mungu lakini pia juhudi zake hazikuzaa matunda.

                              Umeona balaa hili la Selembe na Santo wamewekwa mtu kati? 







 Barbosa na Santo kila mmoja akiwa tayari kutoa msaada kwa mwenzie. 

 
 Langoni kwetu hapa kuna kipindi kama dakika kumi tulikuwa tunashambuliwa.

 Tamim akijitahidi kuondoa hatari langoni.


Sudi akikimbilia mpira usitue kwa adui.

No comments:

Post a Comment