Angalia majukwaa haya, ati hili ndilo jukwaa kuu, si balaa hili. Maana mwanadamu ukiangalia mpira inabidi ukae na gogo aweza kutokezea nyoka pia.
Bawazir huyu akiwa amefumba macho akiogopa kuumwa na nyoka. Maana nilimwambia kaa nikupige picha ili isiwe 'dead picture' naam kitaalam ukipiga picha bila kuwepo mtu inaitwa picha iliyokosa uhai. Lakini alikuwa akiogopa labda anaweza kuumwa na tandu.
Hivi ni vyoo.. Ukitaka kuenda chooni mpaka mtu akusindikize unaweza kukutana na kenge bure.
Jukwaa hili ndilo la wageni rasmi aka waheshimiwa, sasa ikiwa jukwaa la waheshimiwa lipo hivi huko kwengine kukoje?
Huu ni mlango wa upande wa kulia mwa uwanja, ni sehemu ya kukatishia tiketi angalia majani yalivyoota, hapo juu ya kibanda ukipanda maharage unavuna gunia zima.
No comments:
Post a Comment