Mmiliki wa hoteli za JB Belmont Jastus Bagumu amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa wanafamilia wa mzee JB alifariki ghafla leo asubuhi alipokuwa jijini Dar es Salaam ambapo hoteli zake pia zipo.
Mzee JB wa pili kutoka kushoto akiwa na viongozi wa Coastal Union katika hoteli yake mjini Mwanza iku ya jumamosi tarehe 9 feb baada ya mechi dhidi ya Toto Africa; haya ndiyo maneno yake ya mwisho kwa viongozi wa timu "The team played excellent except scoring, i will do something about it," alisema.
Kwa mujibu wa Technical Director Nassor Binslum, maneno ya mzee JB yalimaanisha kutaka kuisaidia timu ya wagosi wa kaya kupata wachezaji wa kulipwa ambao watakuwa wa kipekee kwenye ligi kuu Tanzania bara.
Hakika timu yetu imempoteza mtu muhimu sana katika maendeleo ya soka Coastal Union na Tanzania kwa ujumla.
Mzee JB alikialika kikosi cha Coastal Union kupata chakula cha usiku mjini Mwanza baada ya mechi dhidi ya Toto Africa tarehe 9 mwezi huu.
Hapa Mzee JB akiwa na kikosi cha Coastal Union pamoja na viongozi, JB au Justus Bagumu amesimama katikati ya kocha msaidizi Ally Kidi na mzee Bawazir. Kama hujaelewa hesabu mtu wa tano kutoka kushoto alipo Gabriel Barbosa. amevaa shati la rangi ya kijivu lina mistari.
Mungu ailaze mahala pema roho ya mzee wetu mahala pema.
COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
12/02/2013
Kagera, Tanzania
No comments:
Post a Comment