Ulisikia ile habari ya kidojembe kutaka kuachwa na ndege? Basi TD akazipata tatizo lilikuwa boarding pass, aaahahaaaa sasa hapo wakati nampiga picha uwanja wa kirumba akanambia umeiona boarding pass? bila hii hupandi ndege... ahahaaaa...
Mwarabu kweli anaipenda Coastal Union, mtu katoka taangaaaa kaifuata Coastal Mwanza na jumatano ameahidi atakwenda Bukoba. Jamani Coatal mara nyingine mutoe raha kwa watu kama hawa kwa kuwapa ushindi, ili asione kapoteza shughuli zake burebure... taraaa jamani.
Mwenyekiti Aurora ataniua ati mtu ukikaa meza kuu lazima ujiafanye upo bize ahahaaaaa.
Edo Kumwembe pia alikuwepo, Kirumba ilijaa wadau wa Coastal Union, huyu ndie msemaji wa Coastal Union. Anaitangaza timu kimataifa.
Dah hili zengwe kweli, yaani huyu jamaa mechi inatakiwa kuanza bado anaweka chokaa kwenye mistari.
Huyu jamaa wa katikati kutoka toto Africa nimeambiwa ati aliwahi kuchezea Coastal Union. Kw amnaomfahamu hebu nikumbusheni.
Jamani Shaaban Kado ni golikipa wacheni mchezo....
Benchhi la Coastal hili..
Mgeni Rasmi akisalimiana na kocha wa Coastal Union Hemed Morroco, hili nalo ni zengwe ina mana timu imekosa jacket la kumpa kocha mpaka anavaa la Real Madrid? Mh....
No comments:
Post a Comment