Thursday, March 21, 2013

Coastal Union, Milovan waanza mazungumzo



Jessca Nangawe 
Dar es Salaam. Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umeanza mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Simba Curkovic Milovan kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo msimu unaokuja wa Ligi Kuu. 

Kocha wa sasa, Hemed Morocco mkataba wake unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu, na kama watamalizana vizuri na Milovan basi huenda akawa kocha wao mpya mwakani. 

Afisa habari wa Coastal Union Edo Kumwembe alisema jana kuwa, tayari wamefanya mazungumzo na kocha huyo. 
Kumwembe alisema, mazungumzo ya awali yanaonyesha kuwa yuko tayari kujiunga na Union msimu ujao. 

Milovan alionyesha nia ya kuifundisha Coastal na sisi hatuna pingamizi naye kwani kocha wetu Morocco anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, alisema Kumwembe. 

Aliongeza:
Tunataka mazungumzo yetu yamalizike mapema ili kama kuanza kazi aanze mara tu msimu utakapomalizika. Tunamfahamu vyema Milovan ni kocha mzuri, atatufaa kuijenga timu yetu. 

Milovan ameifundisha Simba katika vipindi viwili tofauti, ambapo mara ya mwisho alitimuliwa mwishoni mwa mzunguko wa kwanza ligi.
Chanzo: Gazeti mwanaspoti.

No comments:

Post a Comment