Sunday, March 10, 2013

Simba wameanza kufufuka baada ya kutembelewa Hospitali na Coastal Union. Matokeo Simba SC 2-1 Coastal Union SC.

Coastal Union wameendelea kujikita katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kupoteza mchezo wa leo dhidi yaa wekundu wa msimbazi Simba kwa bao 2-1 uwanja wa Taifa jijini.

Simba wamerejesha matumaini baada ya kamati ya ushindi inayoongozwa na malkia wa nyuki Rahma El Kharoos, kuzaa matunda kwa kushinda mechi ya kwanza katika nane walizopanga mkakati wa kushinda.

Wagosi wa kaya wana haki ya kujilaumu kutokana na kupoteza nafasi nyingi za wazi hasa baada ya Simba kuchezesha kikosi cha pili ikiwa ni mikakati yao ya kuepuka kuhujumiwa. Lakini mabao mawili ya harakaharaka yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Mrisho Ngassa dakika ya 47 na Haruna Chanongo dakika moja baadae kabla ya refa kupuliza kipenga cha kukamilisha kipindi cha kwanza, yalivuruga kabisa ndoto za wagosi wa kaya kupaa nafasi moja juu..

Coastal Union walikwenda mapumziko wakiwa kichwa chini wakiwa nyuma kwa magoli mawili hali iliyomfanya kocha Hemed Morroco kuzungumza maneno makali katika vyumba vya kubadilishia hali iliyoamsha ari ya ushindi kwa vijana wa Tanga.

Razak Khalfan, alifunga bao la kwanza dakika ya nne tu baada ya kipenga cha kipindi cha pili kuanza baada ya kazi nzuri ya Ibrahim Twaha 'Messi' ambae aliingia kipindi cha pili. hivyo matokeo kubadilika na kuwa 2-1.

Wachezaji walioanza kipindi cha kwanza Coastal Union ni: Shaaban Kado, Hamad Juma, Abdi Banda, Philip Mugenzi, Mbwana Kibacha, Razakh Khalfan, Mohammed Sudi, Suleiman Kassim 'selembe', Joseph Mahundi, Danny Lyanga na Gabriel Barbosa.

kipindi cha pili alitoka Joseph Mahundi na Danny Lyanda, nafasi zao zikachukuliwa na Castro Mumbala na Ibrahim Twaha 'Messi'.

Kikosi cha Simba kilikuwa ni Abel Dhaira, Nassor Masoud 'Cholo', Miraji Adam, Hassan Khatib, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail, Abdalllah Seseme, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa.

Kwa matokeo ya leo Simba wamejiongezea point tatu na kuwa juu zaidi nafasi ya tatu kwa point 34, wakiwaacha wagosi wa kaya wakiwa na point zao 31 katika nafasi ya nne huku wakiwa na mashaka kuendelea kubaki katika nafasi hiyo kwani timu za Kagera Sugar yenye point 31, Mtibwa Sugar point 31 na Ruvu Shooting point 30 wanaimezea mate nafasi ya nne aliyokuwa nayo Coastal Union. 

COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
10 March,2013
Dar es Salaam, Tanzania.


No comments:

Post a Comment