Mwalimu Hemed Morroco anapenda sana mpira wa darasani, akiingia uwanjani ana kauli moja 'mchezaji cheza kama nilivyokufundisha halafu onyesha uwezo binafsi'.
Admin wetu alichelewa kufika Turiani, alifika dakika chache kabla ya timu kuondoka kambini kuelekea uwanjani.
Vijana wakipasha kuondoa uchovu wa safar na ushinda hofu, maana mechi ilikuwa ngumu kama fainali.
Ally Mohammed 'Kidi' kocha msaidizi wa Coastal Union mwenyewe anasema 'mie Polisi sizungumzi sana vtendo tu'.
Shaaban Kado alikuwa na wakati mgumu sana kushndana na mashabiki wake wa zamani, kwani walikuwa wakimzomea uwanjani ati ni msaliti kwa kuiwacha Mtibwa Sugar na kukimbilia Coastal Union. Ila kama kawaida yake uzoefu ulimsaidia sana.
Kit Manager Mohammed, juzi alikuwa na furaha maana ana moyo mlaini sana. Timu ikifungwa analia. mahaba mabaya.
Kocha Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar wa kwanza kulia akiwatazama vijana wake, huyu ni mnazi wa Mtibwa mbali ya kuwa mwajiriwa lakini Mtibwa ndiyo iliyomlea hata akawa nahodha wa Taifa Stars kwa kipindi kirefu.
Meneja wa timu Akida, akiwatazama vijana wake wakipata kumbukumbu ya Turiani Madizini.
Raha ya Mpira ni kujua kuwa soka ni burudani, manahodha wa timu zote wakipeana mikono kuashiria 'Fair Play'.
No comments:
Post a Comment