Nsa Job akifanyiwa vipimo kuangalia athari ya goti lake la kushoto ili kuonenaka atatibiwa vipi.
Nsa Job akiwa nchini India baada ya kufanyiwa Matibabu kwa saa nane mfululizo na hapo yupo fiti.
Vyombo vya habari viliripoti kwa sana suala la Nsa job mshambuliaji hatari nchini kupelekwa India kwa gharama za timu.
Hii ni siku aliyoumizwa vibaya tarehe 28 October, 2012 uwanja wa Chamazi Coastal Union ilipocheza na JKT Ruvu mzunguko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Saa hiyohiyo alipakiwa kwenye gari na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi. Kabla ya kupelekwa India siku chache zilizofuata.
Hii picha ilipigwa saa chache kabla ya timu kuelekea uwanjani kupambana na Simba SC tarehe 10 March wiki iliyopita. Suala lililokuwa likizungumziwa hapa Meneja wa timu Akida alievaa nguo nyekundu, alimfikishia malalamiko mkurugenzi wa ufundi Nassor Mohammed 'Binslum' alievaa shati jeupe kuhusu mchezaji Nsa Job alieipa mgongo Camera. Arudi kambini mjini Tanga kwani anaonekana ameshakuwa fit.
Sasa tujadili pamoja, ikiwa timu imemsusa na haina haja nae Meneja Akida angekuwa na haja ya kumfikiria arudi kambini?
Coastal wakana kumtosa
Nsa Job
NA SOMOE NG`ITU
18th March 2013
Uongozi wa timu ya
Coastal Union ya jijini Tanga umekanusha taarifa za kumtelekeza mshambuliaji
wake,Nsa Job na pia ikisema nyota huyo ana mkataba na klabu hiyo hadi Mei
mwakani. Akizungumza na gazeti hili msemaji wa Coastal Union, Eddo Kumwembe,
alisema kuwa wanasikitika kusikia taarifa za kumtelekeza Job wakati uongozi
unampa huduma zote muhimu kama wachezaji
wenzake wanavyopata licha ya kutocheza.
Kumwembe alisema kuwa Job ambaye alipelekwaIndia na timu hiyo kwa ajili ya
upasuaji, analipwa mishahara yake kila mwezi na pia motisha.
Alisema pia mmoja wa viongozi wa timu aliyeko jijiniDar es Salaam , Nassor Binslum, amekuwa akimpa
fedha kwa ajili ya kwenda hospitali kila anapohitaji kufanya hivyo.
''Ukweli ni kwamba uongozi wa Coastal unashangazwasana na taarifa hizo ambazo kwa upande mmoja
au mwingine inasemekana Nsa mwenyewe anachangia kuzisambaza,'' alisema
Kumwembe.
Aliongeza kwa kusema kwamba uongozi unamkaribisha mshambuliaji huyo kwa mazungumzo ya kuvunja mkataba wakekama
anafikiria kufanya hivyo. Pia alimaliza kwa kuwataka wachezaji wa Coastal wenye
mikataba kutozungumza na vyombo vya habari bila ya ruhusa ya klabu. Nsa
hakupatikana kuzungumzia suala hilo .
Kumwembe alisema kuwa Job ambaye alipelekwa
Alisema pia mmoja wa viongozi wa timu aliyeko jijini
''Ukweli ni kwamba uongozi wa Coastal unashangazwa
Aliongeza kwa kusema kwamba uongozi unamkaribisha mshambuliaji huyo kwa mazungumzo ya kuvunja mkataba wake
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment