Hii ndiyo ratiba
ya mechi zilizobaki Coastal Union ligi kuu mzunguko wa pili. Tarehe 30 March
tunacheza na African Lyon DSM. Tarehe 10 April, tunacheza na JKT Ruvu Tanga.
Tarehe 27 April, tunacheza na Azam FC Tanga. Tarehe 1 May, tunacheza na Young African
DSM. Na tarehe 18 May, tunacheza na Polisi Morogoro mjini Morogoro.
Coastal Union imebakisha mechi hizi ikiwa na point 32 nafasi ya nne, lakini ili kujihakikishia kubaki nafasi nne za juu ni lazima kushinda mechi zote ama kushinda mechi tatu muhimu za Azam FC kwakuwa inachezwa nyumbani, Arican lyon na vibonde wenzao wa Polisi Morogoro. JKT Ruvu wao ni wazuri, ila kwakuwa wanakuja nyumbani lazima watulizwe.
Yanga hata wao wanafungika ingawa wanacheza kwao, ila wana fitina nyingi sana za nje na ndani ya mchezo. Tukipata suluhu pia si mbaya lakini tunataka ushindi kutoka kwao.
COASTAL UNION
DAR ES SALAAM, TANZANIA
26 MARCH, 2013
No comments:
Post a Comment