Tuesday, March 12, 2013

Habari Picha mchezo wa jumapili simba Vs Coastal Union ambapo tulilala 2-1.

 Twaha Ibrahim 'Messi' akitafuta njia za kumtoka Nassor 'Cholo' wa Simba huku Abdi Banda akiwa tayari kumpa msaada Ibrahim.

 AAaaaaaaaaa Mohammed Miraji akikimbilia mpira huku Mohammed sudi akiwa amekata tamaa...

 Wachezaji wa Simba walikuwa wanakaba watatu watatu baada ya kipindi cha pili kuanza maana walielemewa sana na vijana wa coastal ila tatizo umaliziajiiiii.....

 Barbossa alikuwa hataki mchezo, ingawa alitoka eda ya kadi nyekundu aliyoipata Kagera lakini hakujali.

 Dhaira golikipa wa Simba akidaka mpira uliopigwa kwa kichwa dhaifu na Gabriel Barbossa.

 Hamad Juma 'Basmat' alikipiga sana katika mechi hii ingawa aliniudhi dakika za mwanzo kipindi cha kwanza alikosa goli yeye na kipa.


 Castro Mumbala alieingia kipindi cha pili alijitahidi sana kuleta mishemishe katikati ingawa mambo hayakuwa mazuri.

 Shomari kapombe alikuwa na kazi kubwa ya kuwadhibiti wachezaji wa Coastal Union wasivuke ngome yake.

Huyu ni mchezaji wa Simba Jonas Mkude, Aliumia pamoja na philip Mugenzi, alipoteza fahamu kwa dakika tano. ingawa baadae alizinduka ila hakuweza kuendelea na mchezo.

picha zinaendelea...

No comments:

Post a Comment