Sunday, March 17, 2013

Jana mpira ulichezwa uwanjani huku nje ya uwanja mashabiki waliotoka Tanga wakivamia ngoma za watu...

 Watu wanacheza mpira huku kigoma cha Coastal Union kimevamia kigoma cha Mtibwa Sugar, Pius yu teleeeee hapa.

 Rajab Mohammed akimiliki mpira huku Ibrahim Twaha akitafuta mbinu za kuuiba akimbie nao.

 Gabriel Barbosa akijitahidi kukimbia kwa nguvu zake zote kuuwahi mpira uliopigwa na Danny Lyanga (hayupo pichani).

                                                     AAahhhhhhh Baba Nzori weeeee.....

 Wadau wa Coastal Union wakiangalia kwa makini mchezo wa jana, watu wana moyo na timu balaa.

 Jamani mtaona kama huyu mtoto nampendelea lakini ilikuwa kila nikiinua Camera basi lazima amekaa mkao mzuri wa kupigwa picha. Waandishi wanapenda picha zinazozungumza.... Mtanisamehe...


 Beki wa Coastal Union Phili Mugenzi akilalamika baada ya pasi aliyodhamiria kumpa Gabriel Barbosa kudakwa na mchezaji wa Mtibwa.

 Abdi Banda alieingia kipindi cha pili akipga kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda. Unajua nini, alinambia nimpige picha kisa amevaa mnyama (kiatu) mpya.

Danny Lyanga akikokota mpira pembezoni mw uwanja huku beki wa Mtibwa akiwa tayari kuzuia madhara yoyote yatakayosababishwa na Danny.

Makocha wa timu zote mbili wakipongezana kwa suluhu ya 1-1 baada ya dakika tisini za mchezo kuisha.

No comments:

Post a Comment