La Kapiteni Mbwana Kibacha akipeana mkono na Nahodha mwenzie wa Mtibwa Sugar kabla ya mchezo ulioshia kwa suluhu 1-1.
Timu ya
Coastal Union kesho inashuka dimbani kumenyana na African Lyon kwenye uwanja wa
Azam Complex Mbande jijini Dar es
Salaam .
Wagosi wa
kaya wanacheza mchezo wao wa 21 katika ligi ambao unakuwa ni mchezo wa tisa kwa
mzunguko wa pili wa ligi hii ya Vodacom Tanzania Bara; ambapo kauli mbiu ya
mechi ya kesho ni ushindi lazima kwani kwa kufanya hivyo itakwea mpaka nafasi
ya tatu na kuwa na nafasi nzuri ya kubaki kwenye nafasi hiyo mpaka msimu
unaisha ikawa watashinda mechi nne zilizobaki kukamilisha msimu wa 2012/2013.
African Lyon
ambao wapo katika nafasi tatu za chini wapo katika hatihati ya kushuka daraja
msimu huu hawatarajiwi kuleta madhara yoyote kwa wagosi ingawa mpira wa miguu
hautabiriki wala haugangwi, hivyo matokeo yoyote yanaweza kutokea ikiwa wachezaji
hawatotumia vema nafasi watakazopata kwani kwa mujibu wa kocha mkuu wa wagosi Hemed
Morroco, wachezaji wapo fiti kwa mchezo.
Itakumbukwa
huu ni mchezo wa tatu wenye ‘presha’ kwa vijana wa Tanga kwani mchezo wa kwanza
ulikuwa ni dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba ambapo laiti wagosi wangeshinda
mchezo ule basi wangeshika nafasi ya tatu, lakini kwa bahati mbaya wakapoteza
mchezo ule kwa mabao 2-1.
Mchezo wa
pili ulikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu Turiani, ambapo wagosi
wangeshinda mchezo ule wangekuwa na point 34 sawa na Simba lakini vijana
wakaishia kutoa suluhu ya 1-1 hivyo kupata point 32.
Aidha
kutokana na Simba SC kushindwa mchezo wa jumatano Machi 27 uwanja wa Kaitaba
dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-0, nafasi ya tatu inayoshikiliwa kwa muda na
wekundu hao wa msimbazi wanaoandamwa na migogoro kwenye timu yao kiasi
wachezaji na wapenzi kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao, imekuwa wazi
kwa timu tatu za Kagera Sugar wenye point 34, Mtibwa Sugar wenye point 32 na
Coastal Union wenye point 32.
Hivyo lazima
wachezaji wa Coastal Union kupitia nahodha wao Mbwana Kibacha, kutambua macho
ya wakazi wa Tanga yote yapo miguuni mwao kuhakikisha heshima ya soka inarudi
mkoani mwetu kwa kushinda mechi ya kesho tena kwa magoli mengi ili kuepuka
kuandamwa na mahasimu wetu Simba
SC , Mtibwa Sugar na Kagera Sugar
wanaoonekana kuitaka kwa kasi zote nafasi hiyo.
COASTAL UNION
29 March,
2013
No comments:
Post a Comment