Hili gari limekula viama sana, inabidi sasa uongozi uzidishe juhudi msimu ujao timu ipate gari kubwa.
Ahahahaaaa hii picha ilinifurahisha sana Mwalimu Hemed Morroco anapiga darasa huku mkurugenzi wa Ufundi akiwa pembeni akipiga mufela huku anasikiliza kwa jaaaaam.... Ahahhaaaaaa mwenye hela hanuniwi wewe...
Hii picha ilinishawishi kuipiga tu, lakini hata mimi imenishinda kuiandikia maelezo. Hapa anaonekana Meneja wa timu Akida Machai, Mkurugenzi wa ufundi Nassor na mchezaji wa Coastal Union Nsa Job, muda mfupi kabla ya kuelekea uwanjani. Hebu mwenye maelezo ya kutosha anitumie inbox.
Unaweza kujua wawili hawa walikuwa wanazungumza nini?
Hizi ngoma zimesafiri kutoka Tanga kwa kazi moja tu. Kuwanyamazisha wana kidedea, lakini baada ya mechi kuisha zilionekana nzito. Chezeyaaa kufungwa wewe.
Kushoto Meneja wa timu ndogo Ubinde pamoja na mwenyekiti wa hamasa Wandi muda mfupi kabla ya kuelekea uwanjani jumapili iliyopita.
No comments:
Post a Comment