Mechi za leo ligi kuu ya
Vodacom Tanzania
bara mzunguko wa pili ni Simba dhidi ya Toto African, Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa sugar, Ruvu Shooting dhidi ya Azam FC, JKT Oljoro dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Morogoro dhidi ya Yanga, na Coastal union dhidi ya African Lyon.
Kama tulivyotangulia kusema
jana mechi ya leo ni ngumu na tunahitaji ushindi kwa hali na mali, kwasababu
mahasimu wetu wote wanashuka dimbani leo, yaani Simba ambao wanacheza na Toto
African mjini Mwanza, Kagera Sugar wanacheza na Mtibwa Sugar Bukoba uwanja wa
Kaitaba.
Hivyo ili Coastal Union
tukamate nafasi ya tatu ni lazima kushinda mechi ya leo hata kwa goli moja ili
tupate point tatu muhimu zitakazotupatia point 37.
Hata hivyo lazima tuombe
mabaya kwa Simba SC wafungwe au watoe suluhu mechi ya leo ili
wabaki na point 34 hizohizo au 35. halafu Kagera Sugar wafungwe na Mtibwa Sugar
wenye point 31 ama watoe suluhu ili wabaki na point 34 au 35.
Naam hili ni jambo la kawaida
sana katika mchezo
wa soka kuombeana mabaya, si dhambi bali ni kanuni za kisoka kukusanya point
nyingi iwezekanavyo na kuomba mpinzani wako apoteze point nyingi iwezekanavyo.
Ligi bado ni ngumu kwani hata
hao Yanga wanaotajwa kuwa mabingwa wakiwa na point 48 bado wana kazi ngumu ya
kushinda mechi zote tano walizobakisha kwani hata Azam FC wenye point 40 wana
nafasi kubwa ya kushinda mechi walizobakisha, ingawa Simba wanaojikongoja
wameshapoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao ndiyo maana tunaminyana nao
katika nafasi ya tatu.
Mungu ibariki Tanga Mungu
ibariki Coastal Union katika mchezo wa leo dhidi ya vibonde African Lyon uwanja
wa Azam Complex Mbande jijini Dar es
Salaam .
COASTAL UNION
30 March, 2013
No comments:
Post a Comment