Mzee Kines akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na sakata la kujiengua baadhi ya viongozi wa Simba na matokeo mabaya ya timu hiyo kwa mechi za kitaifa na kimataifa.
Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelu 'Julio' akizungumza na wanahabari kuhusiana na mechi ya jumapili dhidi ya Coastal Union kutoka Tanga.
Mabingwa watetezi ligi kuu ya
vodacom Tanzania bara Simba SC ,
wameunda kamati maalum ya ushindi iliyo chini ya uenyekiti wa malkia wa nyuki
El Kharus kabla ya kukutana na wagosi wa kaya siku ya jumapili hii.
Akitoa taarifa hizo ofisi za
timu hiyo mtaa wa msimbazi katika mkutano na waandishi wa habari mchana huu
kaimu makamu mwenyekiti Joseph Itangale ;Mzee kines’ alisema baada ya kujiengua
makamu mwenyekiti Godfrey Nyange ‘Kaburu’ na mwenyekiti wa kamati ya usajili
Zacharia Hans Poppe timu ya Simba bado ipo imara ya tayari imeunda kamati ya
ushindi.
“Sisi hatuna matatizo, hao
walioamua kujiondoka kwenye uongozi watabaki wanachama wa kawaida na kwa
kudhihirisha hilo
leo jioni tutakwenda kurudisha uhusiano wetu na tawi la mpira pesa.
“Timu ipo imara na
tutahakikisha mechi nane zilizobaki kukamilisha msimu Simba tunashinda zote
chini ya kamati ya ushindi inayoongozwa na Rahma Al Kharoos,” alisema mzee
Kines.
Nae kocha msaidizi wa Simba Jamhuri
Kihwelu ‘Julio’ amesema timu yake imejiandaa vizuri na anawaahidi mashabiki wa
Simba wasivunjike moyo na matokeo mabaya, kwani kujiuzulu siyo dawa ya kuondoa
matokeo mabaya.
“Nimesikia Coastal Union
wanasema watatufunga mapema wana haki ya kusema hivyo maana nao wapo ligi kuu
na sisi tutacheza mpira mzuri maana wachezaji wote 25 wapo katika hali nzuri na
11 watakaopata bahati ya kuanza kikosi cha kwanza tuna hakika watacheza vizuri.
“Sote tunamtegemea Mungu na
tunamuomba, kubahatika ama kutobahatika yote ni mipango yake. Hakuna haja ya
kumlaumu Mungu kwa matokeo mabaya maana kuna watu wanamuomba Mungu tangu
wamezaliwa lakini hawajawahi kuokata hata laki moja lakini hawakati tamaa,”
alisema Julio.
Julio aliongeza “Mimi ndie
kocha bora baada ya kufariki Mzirai na kama
huamini angalia timu zote nilizowahi kufundisha namna mafanikio waliyopata.
Hivyo najiamini na ninaamini mechi ya Coastal Union tutashinda.”
Timu ya Simba itacheza na
Coastal Union kutoka Tanga katika uwanja wa taifa siku ya jumapili tarehe 10
mwezi huu katika mechi ya ligi kuu ya voadacom Tanzania bara ambapo mshindi wa
mechi hiyo ndie atakaeshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wenye timu 14.
Simba inacheza mchezo wake wa
19 wakiwa na historia ya matokeo mabaya hivyo mashabiki wa soka Tanzania wanaamini wekundu hao wa mtaa wa
msimbazi walioanza kucheza soka mwaka 1936 wana kazi kubwa ya kurudisha heshima
yao kisoka na
kutetea ubingwa walioupata msimu uliopita.
COASTAL UNION
8 March, 2013
No comments:
Post a Comment