Saturday, March 30, 2013

Yaani leo sitaki kuzungumza kitu chochote, kufungwa 1-0 na African Lyon kumeninyima raha sana.

 Wachezaji wa coastal Union walikuwa wakiingia mpaka golini lakini hata sijui kwanini hawakutumia vema nafasi hizo.

 Selembe hapa akiwa ameweka gambani mpira ambao alitakuwa kumuachia Barbosa halafu yeye akatanua.

 Barbosa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa African Lyon katika mechi ya leo uwanja wa Azam Complex.

 Amani Kyata wa African Lyon akimiliki mpira mbele ya Ibrahim Twaha na Danny Lyanga huku Abdi Banda akiwa tayari kutoa msaada.

 Mchezaji wa African Lyon Sunday Bakari akionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa leo baada ya kumchezea madhambi Joseph Mahundi.

 Ibrahim Twaha 'Messi' akijaribu kushindana nguvu na mpira uliopigwa na Yusuph Chuma ingawa hakuupata.





 Kikosi cha Coastal Union kilichoanza leo dhidi ya African Lyon ambapo walilala 1-0.

 Kikosi cha African Lyon kilichokiadhiri kikosi cha wagosi wa Kaya leo.

Mpira ukionekana kukimbilia wavuni baada ya adhabu ndogo iliyopigwa na Gabriel Barbosa kipindi cha kwanza ingawa golikipa wa African Lyon Abdul Seif aliuwahi.

Mashabiki wa Coastal Union wakijadiliana cha kufanya baada ya kufungwa mchezo wa leo ambao ulikuwa ni muhimu kushinda.

COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
30 March,2013

No comments:

Post a Comment