Wednesday, August 7, 2013

Jinsi Yayo alivyotua Tanga.

Hapa akiwa ndani ya gari baada ya kupokewa uwanja wa ndege wa Tanga, Majani mapana.
 Waliokwenda kumpokea miongoni mwao alikuwepo Seif, hapa akimsindikiza kuingia kambini Raskazone Hotel.

Yayo Lutimba Kato, akiwa nje ya kambi Coastal Union Raskazone Hotel leo asubuhi. Kwa mujibu wa meneja wa kambi Ally Ahmed 'Kiraka' Yayo amewekwa chumba namba 1 pamoja na Crispian Odula kutoka Kenya.

Picha zote kwa hisani ya Miraji Wandi 'Shoka'

Tuesday, August 6, 2013

Yayo Lutimba Joins Coastal Union


August 6, 2013
Yayo Lutimba has today completed a move from URA SC to Tanzanian premier side Coastal Union SC based in Tanga-Tanzania. Yayo Lutimba joined URA SC on June 30, 2012 as a free agent from Express FC after completing a successful season of Bell Super League 2011/2012 where his effort assisted Express FC to clinch the league Championship.
Coastal Union SC developed interest in the former left winger of URA SC during a pre-season tour in Dar-Es -Salaam where URA SC gunned down Tanzanian giants Simba SC 2-1 courtesy of a brace from Yayo Lutimba. 
URA SC further drew with another Tanzanian giant Yanga SC 2-2 in the match where YAyo Lutimba again scored the two goals. Yanga SC then developed interest but backed down when they were advised to formally contacting URA SC with a request for transfer of the player.
The pre-season tour ended in Tanga where Yayo Lutimba’s new Club (Coastal Union SC), who had earlier also scouted him in Simba and Yanga matches against URA SC come up boldly by fulfilling the per-requisite of handing a formal request for transfer of the player to their side.
Speaking shortly after the completion of the deal at Hotel Africana today’s morning, Yusuf Akida Saad, the team manager of Coastal Union SC expressed his joy over the signing of the “star winger” who proved to Tanzanian sides his mighty during the pre-season tour.
Both URA SC and Coastal Union further came to an agreement of a condition that, should the player transfer from Coastal Union to any other club either locally (within Tanzania) or internationally, URA SC will realize a 20% disbursement on the eventual transfer fee paid to Coastal Union SC by any acquiring club at any given time.
Yayo featured on U-20 National team last year 2012 playing matches against Mozambique under Coach Paul Nkata now Head Coach URA SC.
Source: URA facebook page.

Yametimia...

Meneja wa Coastal Union Akida Machai (kulia) akiwa na Yayo Lutimba Kato (katikati) pamoja na mkurugenzi wa ufundi Coastal Union, Nassor Ahmed 'Binslum' baada ya Kato kuingia mkataba wa kuitumikia Coastal kwa miaka miwili.
Hatimaye Coastal Union wamefunga pazia la usajili kwa ajili ya ligi kuu ya soka Vodacom msimu ujao baada ya kumsajili mshambuliaji kutoka Uganda aliyeziteza timu kubwa Tanzania.

Aliyefanikisha zoezi hilo ni meneja wa Wagosi, Akida Machai ambaye amepanda ndege mpaka jijini Kampala kunasa saini ya kijana mdogo mwenye miaka 19, Yayo Lutimba Kato kutoka timu ya mamlaka ya mapato Uganda (URA).

Nassor Ahmed ‘Binslum’, ambaye ni mkurugenzi wa ufundi amesimamia kwa kiasi kikubwa kufanikisha usajili wa wachezaji takriban tisa ukijumlisha na Kato amezungumza na blog hii usiku wa leo baada ya Meneja Machai kuenda kumtambulisha Kato kwa Binslum na kuweka wazi kuwa tatizo la ukame wa mabao litaisha kwa wana Mangush.

Itakumbukwa kocha Mkuu wa Coastal Union, Hemed Morocco wiki chache zilizopita wakati wa kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA, aliweka wazi bado kikosi chake kina matatizo ya umaliziaji.

Alibainisha kikosi hicho kipo vizuri kila idara kuanzia golikipa, mabeki na viungo ila hakuna mtu mwenye uchu wa mabao hivyo kuahidi kuwatumia wachezaji haohao kuwafundisha namna ya kuadhiri magolikipa wa timu pinzani.

Ndiyo maana winga Danny Lyanga alikuwa akichezeshwa namba kumi ili kumuangalia uwezo wake wa kupachika mabao lakini hakuonekana kucheza vema kwenye mechi ya URA.

Kwa usajili wa miaka miwili kuitumikia Coastal Union kinda huyu atakuwa na nafasi nzuri sana kujitengenezea jina nchini Tanzania hasa baaada ya kuwa na rekodi nzuri ya kuwafunga Simba na Yanga mabao mawili mawili katika mechi walizokutana nazo kwa vipindi tofauti.

Zipo taarifa kuwa Yanga nao walikuwa mbioni kumnyakua kinda huyu lakini Meneja Akida Machai amewazidi akili kwa kumfuata hukohuko kwao Uganda. Na hizi ni mbinu za ‘kimafia’ zinazotumiwa na timu kubwa duniani kote kunasa wachezaji mahiri.

Mungu akipenda kesho Kato ataungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo pembezoni mwa bahari ya hindi Raskazone Hotel, jijini Tanga.

Wagosi wameanza vizuri mechi zao mbili za majaribio ambapo mechi ya kwanza walishinda bao 1-0 dhidi ya URA na siku tatu baadaye wakashuka dimbani dhidi ya Simba SC ambao nao walichapwa 1-0. Zipo taarifa za kucheza mechi ya kirafiki siku ya Eid pili uwanja wa Mkwakwani lakini zikishathibitishwa na timu tutakayocheza nayo tutawahabarisha.

COASTAL UNION
6 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Monday, August 5, 2013

Kocha wa timu B, Joseph Lazaro afiwa na mkewe.


 

Mke wa kocha mkuu wa coastal Union B, Joseph Lazaro amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Bombo mjni Tanga baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa hiyo kutoka Tanga mwenyekiti wa hamasa Coastal Union, Miraji Wandi amesema mke wa Lazaro alikuwa akisumbuliwa na kiharusi (Stroke) kwa muda mrefu mpaka mauti yalipomfika saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Kocha huyo ambaye amechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu B, Bakari Shime amesema msiba utakuwepo nyumbani kwake Makorora Mzingani na maziko ya kumpumzisha mkewe Bi Farida Mussa, yatafanyika leo saa kumi alasiri kwenye makaburi ya Maftah.

Joseph Lazaro pia aliwahi kuichezea Coastal Union na kuwa chachu ya mafanikio yaliyowafanya wana Mangush kuwa wafalme wa soka Tanzania Bara mwaka 1988.

Mungu ailaze roho ya marehemu Farida Mussa mahala pema peponi Amin.

COASTAL UNION

AGOST 5, 2013

DAR ES SALAAM, TANZANIA

Sunday, August 4, 2013

Chema hakidumu...

Mkurugenzi wa ufundi Coastal Union, Nassor Ahmed Binslum (kulia), akiwa na mchezaji wa zamani wa Coastal Union aliyekuwa katika kikosi cha ubingwa 1988, Idrissa Ngulungu 'Kiraka' (Marehemu).

ngulungu alikwenda kumtembelea Binslum ofisini kwake Mnazi Mmoja mwezi uliopita na kupanga mikakati mingi ya ubingwa msimu unaoanza mwezi ujao. Nguli huyo aliyekuwa akicheza namba zote kasoro golikipa alifariki juzi kwa ajali ya gari mjini Morogoro na kuzikwa jana hukohuko Morogoro.

Msiba wa Idrissa Ngulungu juzi.

Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal (mwenye suti ya michezo) akiwa na ma-lgend wa Coatal Union pamoja na mtaangazji wa Clouds FM Mbiga wa Mbwiguke (mwenye kofia) walipokuwa mjini Morogoro kuhudhuria maziko ya mchezaji wa zamani wa Coatla Union Idrissa Ngulungu 'Kiraka'.

Friday, August 2, 2013

Mallegend 10 wa Coastal Union kumzika Idrissa Ngulungu Morogoro kesho.

Uongozi wa Coastal Union unasikitika kutangaza kifo cha kiungo wa zamani wa klabu hiyo Idrissa Ngulungu (kiraka) aliyefariki leo asubuhi kwa ajali ya gari mjini Morogoro.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Morogoro kaka wa marehemu, Hussein Ngulungu ambaye pia alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa amesema marehemu na ndugu wengine walikuwa wanakwenda kuzika upande wa wakwe zao maeneo ya Kisaki mjini humo.

Kwa maelezo ya Hussein, marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Nissan Patrol pickup walipofika maeneo ya Mikuyuni dereva alikunja kona kali na gari ikamshinda ikagongana na Noah gari aliyokuwemo marehemu ikapinduka mara kadhaa.

Mbali ya Idrissa Ngulungu ajali hiyo inesababisha kifo cha ndugu yao mwingine na majeruhi ambao mpaka sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa za familia zinaeleza kuwa maziko yatafanyika kesho saa kumi alasiri kwenye makaburi ya Kola hapohapo Morogoro.

Idrissa Ngulungu ama Kiraka atakumbukwa na wana Mangush kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa klabu hiyo hasa kuwepo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa soka Tanzania bara mwaka 1988.

Katibbu wa Wagosi wa Kaya, Kassim Siagi anasema Ngulungu alikuja Tanga akitokea Morogoro mwaka 1986 na hakuwahi kufanyiwa majaribio kwani jina la kaka yake Hussein Ngulungu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anachezea timu ya Mseto na timu ya Taifa lilitosha kumpa dhamana ya kuchezea kikosi cha Coastal Union ambacho kilikuwa moto kwa kipindi hicho.

Ngulungu alipachikwa jina la ‘Kiraka’ na wapenzi wa Coastal Union kutokana na uwezo mkubwa wa kucheza namba zote kasoro golikipa tu. Ingawa alikuwa akicheza nafasi ya kiungo wa pembeni lakini kocha mkuu wa wakati huo Zakaria Kinanda (marehemu) alimweka namba nne, namba tatu na mara nyingine alimchezesha kama mshambuliaji lakini alicheza utadhani ndizo namba zake za siku zote.

Kwa upande wake Juma Mgunda ‘Kipande cha baba’ alimuelezea Ngukungu kama mtu mwenye uwezo mkubwa kisoka ambaye hakuwa kumuona.

“Sisi tulimkuta Ngulungu akiwa Coastal Union, nakumbuka alianza mwaka 1984 akitoka timu ya Tabora inaitwa Tindo, walishiriki ligi daraja la pili ndipo viongozi wa Coatal Union wakamuona na kumchukua.”

Naye mchezaji mwingine wa zamani wa Coastal Union, Razak Yusuph ‘Careca’ anamzungumzia Ngulungu kama mtu wa watu na mpenda masikhara sana.

“Nikianza kuelezea sifa za Ngulungu siwezi kuzimaliza, ni mtu wangu wa karibu sana juzi tu katika Ramadhani hii hii alinitumia mizigo kwa ajili ya watoto wake hapa Tanga na kila mechi za Coastal Union alikuwa anakuja, hata mechi ya wiki iliyopita tuliyocheza na Simba aliaka kuja nikamwambia apumzike maana ni mechi ya kirafiki tu asubiri ligi kuu.
“Nakumbuka Coastal Union tulikuwa na tatizo la kiugo wa kati na yeye akikuwa anacheza namba 10, lakini aliichez vizuri sana, baadaye kocha akampanga namba 5 akaonyesha uwezo kuliko namba 5 wote waliowahi kutokea Coastal Union.


“Mwaka 1998 wakongwe wote tuliombwa kuirudisha timu kwenye ligi kuu nilikuwepo mimi (Careca), Abu Yassin Napili, Hilal Hemed, Juma Mgunda, Idrissa Ngulungu, Kolongo, na wengine wengi siwakumbuki kwa sasa. Ambacho naweza kusema ni kuwa Ngulungu angekuwa anacheza sasa sioni wa kumfananisha naye.”

Ujumbe wa Coastal Union ukiongozwa na mwenyekiti Hemed Hilal ‘Aurora’ utaondoka kesho asubuhi kuelekea Morogoro wakiwepo na wakongwe Hussein Mwakuluzo, Juma Mgunda, Razak Yusuf ‘Careca’, Doglas Muhani, Said Salum Kolongo, Mohammed Kampira, wengine kutoka Dar es Salaam ni golikipa wa zamani Mohammed Mwameja, Abuu Yassin Napili, na Aggrey Chambo.

Mechi ambayo haitasahaulika vichwani mwa wapenda soka ni ile ambayo Ngulungu alisababisha kocha wa Yanga kutimuliwa kazi baada ya kupachika mabao mawili katika uwanja wa Mkwakwani.

Ilikuwa ni mwaka 1991 kwenye ligi kuu ambapo Yanga walikuja tanga na kocha mzungu, Ngulungu alifunga mabao mawili peke yake na bao la tatu lilitumbukizwa kimiani na Kingsley. Yanga wakapata bao la kufutia machozi lililofungwa kwa njia ya penati na Aboubakar Salum ‘Sure Boy’.

Baada ya mecho kocha wa Yanga iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Abbas Gulamali ‘Mwana wa Pakaya’ alisema hakutegemea kama watacheza na timu ngumu kama hiyo kwani walikuwa wakiidharau Coastal Union, baada ya kauli hiyo uongozi wa Yanga uliamua kumsimamisha kocha huyo Mzungu kwa madai ya kuwadhalilisha.

Ngulungu mpaka mauti yanamfika anakadiriwa kuwa na miaka 43 amejaaliwa kupata watoto watano ambao wanaishi Tanga na mama yao. Ngulungu na mkewe waliachana na tayari mama watoto wake ameshaolewa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMIN.

CASTAL UNION
3 AGUST, 2013-08-02
DAR ES SALAAM, TANZANIA