Kocha wa Yanga (kulia) Van De Plunm akiwa na Meneja wa Yanga Hafidh Saleh kabla ya mchezo leo.
Abdi Banda akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Yanga, Oscar Joshua katika mchezo wa leo uwanja wa Mkwakwani.
Haruna Moshi 'Boban' akimuonyesha kocha Chipo kuwa mambo anayaweza. |
Kenneth Masumbuko akitolewa uwanjani baada ya kuumia kipindi cha pili.
KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Yusuf Chipo ameanza kuridhishwa
na kiwango cha wachezaji wake mbali ya kutoa suluhu ya pili katika mechi za
ligi kuu Tanzania Bara.
Mechi ya leo kati ya Coastal Union na mabingwa watetezi wa
ligi hiyo Yanga, iliyopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani imeisha kwa sukuhu tasa
ya bila kufungana lakini walimu wote wawili wameonyesha kuvutiwa na soka
lililochezwa leo.
Yanga walianza kwa kasi huku wakilisakama lango la Wagosi wa
Kaya mfululizo na kupata kona Zaidi ya nne ndani ya dakika tano za awali
kipindi cha kwanza. Hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa Coastal Union ambapo
Yanga walionekana kuwa makini na kushambulia kwa kasi.
Dakika ya 36, Crispian Odula wa Coastal Union alikosa bao la
wazi akiwa yeye na golika wa Yanga Deogratius Munishi (Dida).
Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha hakuna mtu alieona lango
la mwenzake hali iliyowapa mwanya makocha kuwapa nasaha ili wasirudie makosa
waliyofanya awali.
Hata hivyo maamuzi ya leo kwa refa wa kati yalionyesha
kuwakera mashabiki wa pande zote mbili halo iliyoleta taharuki na mchezo
kusimamishwa Zaidi ya mara mbili ili kuweka mambo sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kushambulia kwa kasi ili
kupata bao moja ili kuwaharibu kisaikolojia wachezaji wa Coastal Union, hata
hivyo mlinda mlango wa Wagosi, Shaaban Kado alikuwa makini langoni kuhakikisha
hatari zote zinaishia nje ya eneo lake la kujidai.
Dakika tisa za awali katika kipindi cha pili Nadir Haroub ‘Canavaro’
alitaka kujifunga katika harakati kuokoa shuti la Abdi Banda. Baada ya hapo
mashabiki wa Yanga wakaanza kumrushia chupa Canavaro.
Katika kipindi cha pili Yanga walianza kupoteza pumzi na
kuchezewa mpira mwingi na Coastal Union, walioamka kutoka usingizini.
Hata hivyo ilipofika dakika ya 68 mwamuzi alitoa nafasi kwa
Yanga kupiga mpira wa adhabu ndogo baada ya mchezaji wao kuchezewa vibaya nje
kidogo ya 18. Lakini faulo ile ilionekana kuwakera wachezaji wa Coastal Union,
ndipo mwamuzi akampa kadi ya njano Haruna Moshi ‘Boban’.
Baadae dakika ya 77 winga wa Coastal Union, Kenneth
Masumbuko aliumia misuli ya mguu akaingia Mohammed Sudi, ilipofika dakika ya 86
alitoka Yayo Kato akaingia Mohammed Miraji (86).
Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yaliendelea kusomeka
hivyo hivyo 0-0. Hali hiyo ilionekana kuwakera mashabiki wa timu zote kwani
Yanga bado wana kampeni ya kushikilia kileleni, huku Coastal Union wakitaka
kujisafisha baada ya kutoa suluhu ya 1-1 na JKT Oljoro katika uwanja huu huu wa
Mkwakwani Jumamosi iliyopita.
COASTAL UNION
29 JANUARI, 2013
TANGA, TANZANIA
No comments:
Post a Comment