Monday, January 6, 2014

Coastal Union inae kocha wa walinda mlango.

Kocha wa walinda mlango Coastal Union, Adam Abdallah ‘Meja’, akiwa na kocha mkuu wa timu hiyo Yusuf Chipo, wakibadilishana mawili matatu.


Baada ya kuondoka kwa kocha wa walinda mlango Coastal Union, Juma Pondamali ‘Mensah’ watu wengi wamekuwa na maswali kuhusu nani ataziba nafasi yake.
Lakini tunapenda kuwafahamisha kuwa Coastal Union tayari imemnasa mwalimu wa walinda mlango Adam Abdallah ‘Meja’, ambae inawezekana kuwa ndie kocha mdogo wa walinda mlango kuliko wote Tanzania na mwenye uwezo wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Wagosi wa Kaya, Hemed Hilal ‘Aurora’, amethibitisha kumnasa kocha huyo ambae yupo na timu kwa miezi mitatu sasa. Vilevile ndie alieiletea mafanikio timu ya U20 katika michuano ya Uhai Cup mwaka huu kwa kuwafundisha vema magolikipa wa timu hiyo mpaka kutwaa kombe.
Hivyo ifahamike tu kuwa Coastal Union, inae kocha wa walinda mlango hivyo tetesi za kuwa tunatafuta mtu wa kuziba pengo la Juma Pondamali, hazipo.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI COASTAL UNION
JANUARI 6, 2014

No comments:

Post a Comment