Kuna taarifa zimeanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii
kuhusu suala la wachezaji watatu wa Coastal Union, kutaka kuchukuliwa na klabu
moja hapa nchini Oman.
Nikiwa msemaji wa Coastal Union, ambae nimeambatana na timu
nchini hapa naweka wazi kuwa taarifa hizo hazina ukweli. Hakuna kitu kama
hicho.
Nimezungumza na mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’
ambae pia yupo hapa Oman, na ameonyesha kusikitishwa sana na taarifa hizo na
mtoa taarifa aliwahi kumuuliza na alimpa majibu hayohayo kuwa hakuna kitu kama
hicho.
Vilevile imedaiwa kuwa uongozi umeshaanza mazungumzo na
klabu hiyo inayotaka kuwachukua wachezaji watatu, hakuna kitu kama hicho
uongozi haujafanya mazungumzo yoyote na klabu nchini hapa.
Aidha ikiwa kitu kama hicho kipo si vibaya, kwani inaonyesha
ni namna gani wachezaji wa Coastal Union wanacheza soka la kuaminika, lakini
kuzungumza mambo kwa hisia hiyo ni kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.
Hivyo ibaki kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji yeyote
alietakiwa na klabu, lakini ikiwa kuna klabu imeonyesha kuridhishwa na kiwango
cha mchezaji yeyote klabu inaweka wazi milango yake kufanya mazungumzo kwani
hiyo ni kawaida na ni bahati kwa mchezaji na klabu.
HAFIDH KIDO (Msemaji)
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
+986 97695911
No comments:
Post a Comment