TIMU ya Coastal Union jana iliwasili jijini Muscat Oman
usiku saa sita na kufikia katika hoteli ya City Centre.
Kaimu balozi wa Tanzania nchini Oman, ndie alietupokea
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mascut na kutuelekeza vema kuhusu masual
mazima ya mji huo.
Nae mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya
Tanzania, Talib Hilal alikuja hotelini na kuzungumza nasi juu ya masuala mazima
ya soka nchini hapa.
Talib, ndie mwenyeji wetu ambae anaratibu kila tukio
tutakalofanya kuhusu mechi na mazoezi ya timu. Vilevile atahakikisha maisha
yetu mjini Mascut yanakuwa rahisi kwa kusimamia masuala ya usafiri na mambo
yote muhimu.
Kesho saa tisa alasiri timu itashuka dimbani katika uwanja
wa Musanaa ambapo tutacheza mechi ya kirafiki na timu ya Musanaa ambayo ipo
‘top four’ ya ligi kuu ya Oman.
Aidha zipo taarifa zilizotolewa na moja ya gazeti la udaku
juu ya hali mbaya ya maisha kwa timu ya Coastal Union, nchini Oman. Lakini
nadhani picha zinazungumza maneno mengi kuliko maandishi. Hivyo kwa nafasi ya usemaji
nahakikisha kuwa vijana wapo katika hali nzuri na hakuna matatizo yoyote.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara ambae pia ni mwenyekiti wa
Wagosi, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu itacheza mechi nne za majaribio kabla ya
kurudi Tanzania baada ya wiki mbili.
Taarifa nyingine zitaendelea kutolewa kupitia vyanzo vyote
vya Coastal Union……
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
10 JANUARI, 2014
No comments:
Post a Comment