COASTA Union Wagosi wa Kaya, Wagosi wa Ndima, leo watashuka
dimbani dhidi ya timu ngumu inayoshika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Oman,
Seeb Club.
Seeb SC, ambao wamecheza mechi 12 wameshinda mechi sita
kutoa suluhu tano na kupoteza mchezo mmoja hivyo kuambulia point 23, wakiwa
wamepishana point mbili na timu inayoongoza ligi, Al Nahda Club ambayo ina
point 25 ikiwa imecheza michezo 12, kushinda minane, kupoteza mitatu na kutoa
suluhu moja.
Aidha katika mechi ya leo Wagosi watahakikisha wanacheza kwa
umakini ili kuondoka na jina zuri nchini Oman, ambapo mpaka sasa klabu nyingi
zinatuma maombi ya kutaka kucheza na Wagosi baada ya kupata taarifa ya ushindi
wa mfululizo katika mechi mbili za awali dhidi ya Al Mussannah inayoshika
nafasi ya saba katika ligi kuu na Oman Club iliyo daraja la kwanza.
Mechi ya leo itachezwa saa kumi alasiri katika uwanja wa
Seeb Club, jijini Muscat ingawa mratibu wa mechi za Coastal Union nchini hapa
Twalib Hilal, ametoa maelezo kuwa kutakuwepo na mechi ya tano kabla ya kuondoka
Januari 23, kujiandaa na mechi ya ufunguzi mzunguko wa pili dhidi ya JKT Oljoro
katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Itakumbukwa Coastal Union tangu iwasili nchini Oman, januari
9 mwaka huu kwa ziara ya wiki mbili, imeshacheza mechi tatu dhidi ya Al Mussannah
Club, Oman Club na Fanja SC. Ambapo wameshinda mechi mbili kwa mabao 2-0 kila
mechi na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Fanja SC kwa bao 1-0.
Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Coastal Union, Yusuf Chipo timu
yake imepata mambo mengi ambayo yamemsaidia katika mafunzo yake.
“Mbali ya utulivu kwa wachezaji lakini nimejifunza mambo
mengi kutoka klabu za hapa, kuanzia ubora wa viwanja, serikali inavyopenda soka
na vifaa vya kufundishia. Naamini vijana wangu wamejifunza mambo mengi vilevile
na mzunguko wa pili utakuwa mzuri tusubiri,” alisema.
Kikosi cha leo kitakachoanza dhidi ya Seeb Club ni, Shaaban
Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Said ‘Nyoso’, Mbwana Kibacha, Jerry
Santo, Ally Nassor ‘Ufudu’, Haruna Moshi ‘Boban’, Atupele Green, Danny Lyanga
na Yayo Kato Lutimba.
Wengine 12 waliobakia wanaweza kuingia kutokana na upungufu
utakaojionyesha wakati mchezo ukiendelea.
COASTAL UNION
18, JANUARI 2014
MUSCAT, OMAN
+986 97695911
No comments:
Post a Comment