Thursday, January 16, 2014

Fanja SC 1-0 Coastal Union SC

 Kenneth Masumbuko akiambaa na mpira pembeni ya uwanja.

 Danny Lyanga, akituliza mpira huku wachezaji wa Fanja wakitafuta namna ya kumpokonya.

Kama kungekuwa na zawadi ya man of the Match ningempa Danny Lyanga.


Jerry Santo akiminyana kuhakikisha mpira haupoteo, ndiyo akzi ya kuingo.
 Hamadi Juma akijaribu kuuwahi mpira usitoke, hata hivyo alizidiwa kasi na mpira ukatoka.

 Haruna Moshi 'Boban' akiinua macho kuangalia wa kummiminia majaro.

 Atupele Green, akikokota mpira..


 Razakh Khalfan akiwa katikati ya dimba kwa kujiamini.

Jerry Santo akituliza mpira huku Atupele (9), akihakikisha mpira haupotei, yupo tayari kutoa msaada.
 Atupele, akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Fanja SC.

 Mtu Mzima Boban, akimtoka mchezaji wa Fanja SC.

 Wakati ndinga ikiendelea huku nje kulikuwa kunafanyika biashara ya wachezaji.

 Kocha leo alikuwa makini sana maana alijua timu anayocheza nayo itamsaidia kujua ubovu wa timu yake upo wapi.



 Shaaban Kado alikuwa makini lakini lakini bao alilofungwa lilikuwa la kiufundi hakuwa na namna kulikuwa na mtu anaitwa Ely Cisse ndie aliepika bao.

 Al Habsi na Al Baajun wakipozi kwa picha baada ya mechi.

Mashabiki wanazi wa Coastal Union wakipata picha ya pamoja na kocha wa Coastal Union, Yusuf Chipo baada ya mechi usiku huu.

Kikosi cha leo kilicholala 1-0 dhidi ya Fanja Sports Club
Mwenyekiti wa Fanja Sc, El Sumry (mwenye kanzu) akijadiliana mawili matatu na kocha Yusuf Chipo (jaket jekundu) na mwenyekiti Hemed Hilal 'Aurora,' baada ya mechi iliyoisha kwa ushidi wa 1-0 Fanja wakiibuka kifua mbele.



COASTAL Union, leo imekubali kipigo cha ao 1-0 dhidi ya wenyeji wao nchini Oman, Fanja SC inayoshika nafasi ya tano katika ligi kuu ya nchi hii katika uwanja wa Fanja Club.
Bao la Fanja, liliingizwa kimiani mnamo dakika ya 25 na Mohammed Maashari, baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa mshambuliaji hatari wa Fanja raia wa Senegal, ambae alikuwa mfungaji bora msimu uliopita, Ely Cisse ambapo Mohammed alipopokea pasi hiyo alikabiliana uso kwa uso na mlinda mlango wa Wagosi wa Kaya, Shaaban Kado na kuchagua upende wa kushoto Kado akaishia kuukodolea macho mpira ukiingia wavuni.
Baada ya hapo Fanja, waliongeza kasi wakiamini wataongeza bao la pili lakini vijana wa Coastal Union walikuwa makini kuhakikisha hawaondoki na kapu la maao uwanjani hapo. Zilipokaribia dakika chache kuisha kipindi cha kwanza, Coastal Union waliongeza kasi ya ushambuliaji lakini umaliziaji haukuwa mzuri.
Mara nyingi Danny Lyanga na Kenneth Masumbuko, waliingia ndani wakisaidiana na mtu mzima Haruna Moshi ‘Boban’, lakini mpaka mwamuzi wa leo Majid Salim anapuliza kipyenga kuashiria mapumziko bado ubao uliendelea kusomeka 1-0.
Kipindi cha pili Fanja walifanya mabadiliko ya mlinda mlango na wachezaji wengine watatu lakini Coastal Union iliendelea na kikosi chake kilichoanza awali.
Mchezo ulianza kwa kasi huku Fanja wakionekana wamechoka, lakini Wagosi wa Kaya wakaendelea kukosa mabao ya wazi yaliyowaumiza mashabiki wachache waliokuwa nje kuwashabikia.
Ilipofika dakika ya 70 Othman Tamim, alichonga kona upande wa kulia mwa uwanja ambayo ilipita usoni mwa wachezaji wawili wa Coastal Union Masumbuki na Danny, bila kufanya chochote ingawa Nahoda wa Wagosi Juma Nyoso alimbana golikipa wa Fanja ili kuwapa nafasi washambuliaje wake watumbukize wavuni lakini haikuwa hivyo na kukosa bao la wazi ambalo lingekuwa la kusawazisha.
Ilipofika dakika kumi kabla ya mchezo kuisha kocha Yusuf Chipo alifanya mabadiliko kwa kumtoa Atupele Green, akamuingiza Mohammed Miraji, ambae dakika moja baada ya kuingia alimshinda mbio mlinzi wa Fanja akakabiliana uso kwa uso na golikipa wa klabu hiyo lakini akapaisha.
Dakika tano za mwisho Coastal Union walimiliki mpira na kuwachezea Fanja nusu uwanja hali iliyoonyesha matokeo yangeweza kusomeka 1-1 muda wowote, lakini filimbi ya mwisho iliwanyongonyeza wachezaji wa Coastal union.
Kwa matokeo hayo Coastal Union ambao wapo Muscat Oman, kwa ziara ya wiki mbili wamepoteza mchezo mmoja katika minne ambayo wamepanga kucheza wakiwa hapa.
Michezo miwili ya awali walifanikiwa kuibuka kifua mbele kwa kuwachapa mabao 2-0, Al Mussannah Club, inayoshika nafasi ya saba katika ligi ya Oman. Vilevile wakawachapa 2-0 klabu ya Oman Ckub inayosiriki ligi daraja la kwanza nchini hapa.
Mechi ya nne itakayochezwa na Coastal Union ni dhidi ya Seeb Club, inayoshika nafasi ya nne katika ligi ya hapa. Ingawa zipo taarifa kuwa kutakuwepo mechi ya tano, lakini mpaka sasa wenyeji wetu hawajatoa maelezo ya moja kwa moja kuwa itakuwepo ama la.
Baada ya mechi kocha wa Fanja SC, Hisham Gidran alimwambia mwandishi wetu kuwa ameshangaa kuona Coastal Union inacheza soka la kueleweka namna hiyo mbali ya kushika nafasi za chini katika ligi ya Tanzania.
“Inaonekana ligi ya Tanzania imekuwa ngumu, maana mmecheza soka safi sikutegemea, maana nimeona katika msimamo wa ligi mpo nafasi za chini, naamini mtafanya vizuri ikiwa mtacheza namna hii,” alisema.
Nae kocha wa Coastal Union, Yusuf Chipo alipokuwa akishuka kwenye gari kuelekea hotelini alisema hiyo gemu ilikuwa nzuri na ana cha kusema Zaidi ya hicho.
Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Nyoso, Marcus Ndeheli, Jerry Santo, Razakh Khalfan, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga, Haruna Moshi, na Atupele Green. Baadae alitolewa Atupele akaingia Mohammed Miraji.
COASTAL UNION
16 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN




No comments:

Post a Comment