Yusuf Chipo, kocha mkuu wa Coastal Union akisisitiza jambo katika darasa leo asubuhi..
Kocha Msaidizi, Ally Jangalia akifuatilia darasa la Mwalimu Yusuf Chipo, leo asubuhi. |
Ayoub Semtawa, yeye alichelewa kufika, hivyo kila mwalimu akimaliza darasa humfuata kwa muda wake aongeze nondo. |
LEO timu ya Coastal Union itashuka dimbani kucheza mechi ya
kirafiki na timu ya Oman Club, katika uwanja wa Nadi Oman katika wilaya ya
Boshra jijini Muscat.
Hiyo inakuwa mechi ya pili tangu kuwasili Januari 9, mwaka
huu kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili ligi kuu ya Tanzania
bara.
Mechi ya kwanza Coastal Union, walicheza na Al Musannah
inayoshiriki ligi ya Oman, ambapo Wagosi wa Kaya wliibuka na ushindi wa mabao
2-0 ambayo yaliingizwa kimiani na Yayo Kato na Kenneth Masumbuko.
Aidha Wagosi wa Kaya wakiwa hapa watacheza mechi nne ingawa
mwenyeji wetu Twalib Hilal, ametuahidi kututafutia mechi nyingine ya daraja la
chini ili Kocha Yusuf Chipo, aweze kuwajaribu vijana wake wa U20 waliopandishwa
msimu huu.
Timu nne zilizopangwa awali ni Al Musannah Club, Oman Club,
Seeb Club na Fanja Club, timu zote tatu zipo ligi kuu ya Oman, ila Oman Club
inacheza ligi daraja la kwanza ambapo kwa hapa wanaita Professional League.
Kikosi cha leo kitakachocheza na Oman Club, saa kumi na nusu
alasiri ni: Said Lubawa, Ayoub Masoud, Othman Tamim, Marcus Ndeheli, Yusuf Chuma,
Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’,
Mohammed Miraji, na Othman Abdullah ‘Ustadh’.
COASTAL UNION
14 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN
No comments:
Post a Comment