Vijana wa Coastal UNion wakipasha kabla ya mechi dhidi ya JKT Oljoro Jumamosi iliyopita.
Kigoma cha Wagosi wa Kaya kikishughulika katika mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Oljoro.
Angalia uwanja ulivyokuwa mtupu mechi ya Juammosi, haya ni matokeo ya tiketi za Elektroniki. |
Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 29 mwaka huu) tayari yameanza,
hivyo wanatakiwa kununua mapema.
Mechi hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa
Azam Complex.
Kwa washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati
ya Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao
mikononi, hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba
*150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.
Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina
mfumo wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo
wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.
COASTAL UNION
27 JANUARI, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment