Thursday, January 16, 2014

Picha za darasani leo asubuhi.

 Juma Kido, shabiki wa Coastal Union aliewasili usiku wa jana kutoka Dubai. Amekuja kuangalia game ya Fanja SC na Coastal Union ahalafu anarudi.

Kocha mkuu wa Coastal Union, Yusuf Chipo akiwaelekeza jambo wachezaji katika darasa la leo asubuhi kujiandaa na mechi dhidi ya Fanja SC alasiri hii.
Salim Esry, mwenyeji wetu Oman alietusaidia mambo mengi tangu tunawasili januari 9, akiwa na Juma Kido wakisikiliza darasa la Mwalimu Chipo.
eeenhhhhh




Kikosi cha leo kitakachokutana na Fanja Sc, Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Marcus Ndeheli, Juma Said ‘Nyoso’, Jerry Santo, Danny Lyanga, Razakh Khalfan, Atupele Green, Haruna Moshi ‘Boban’, na Kenneth masumbuko.
Mechi itachezwa saa kumi alasiri katika uwanja wa Fanja Club, ambayo itakuwa mechi ya tatu tangu tuwasili Oman kwa ziara ya  wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania Bara.
Mechi ya awali tulicheza na Al Mussannah Club tukashinda 2-0, mechi ya pili tulicheza na Oman Club, tukashinda 2-0.



COASTAL UNION
16 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN

No comments:

Post a Comment