Wednesday, January 15, 2014

Coastal Union kukutana na Fanja FC leo.

BAADA ya ratiba ya kunywa chai saa tatu asubuhi, ratiba ya timu kwa siku ya leo ni darasa saa tano asubuhi kujiandaa na mechi dhidi ya wenyeji wetu Fanja SC, saa kumi alasiri katika uwanja wa Fanja Club, au kwa kiarabu Nadi Fanja.

Hiyo itakuwa ni mechi ya tatu kwa Coastal Union, nchini Oman tangu wawasili Januari 9, mwaka huu kwa kambi ya wiki mbili. Mechi ya kwanza walicheza dhidi ya Al mussannah Club, katika uwanja wa Al Mussannah wakashinda 2-0. Wafungaji wa wakiwa ni Yayo Kato na Kenneth Masumbuko.

Game ya pili ilikuwa dhidi ya Oman Club katika uwanja wa Nadi Oman, Coastal Union wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Mohammed Miraji na Yusuf Chuma.

Aidha baada ya mechi ya leo, dhidi ya Fanja SC, Wagosi watakuwa na mechi nyingine dhidi ya Seeb Club katika uwanja wa Seeb.

Baada ya hapo mipango ya safari itakuwa Januari 23, tutatua uwanja wa ndege wa kimataifa JK saa kumi alasiri.

COASTAL UNION
16, JANUARI 2014
MUSCAT, OMAN

No comments:

Post a Comment