Tuesday, July 2, 2013

Coastal Union kuanza kambi Julai 7, 2013.


Uongozi wa Coastal Union unatoa taarifa rasmi kuwa wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini siku ya jumapili Julai 7 mwaka huu kwa ajili ya kuanza mazoezi kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi Nassor Binslum ambaye ndiye ana mamlaka ya kusimamia masuala yote yanayohusu mazoezi na mikakati ya ushindi dimbani, amesema wachezaji wameshaanza kupewa taarifa juu ya kuanza mazoezi mapema mwezi huu.
“Viongozi wamekaa na wamekubali mazoezi yaanze tarehe 7 mwezi huu, kwa sasa kambi yetu ambayo ni Raskazone Hotel ipo katika matengenezo mpaka itakapofika tarehe saba kila kitu kitakuwa tayari kuanzia wapishi, vitanda na magodoro pamoja na walinzi wa kambi, hivyo ieleweke tu kuwa mazoezi yanaanza mwishoni mwa wiki hii,” alisema Binslum.
Hata hivyo uongozi mbali ya kusajili wachezaji wapya bado haijaweka wazi juu ya wachezaji wa zamani walioacha na waliopelekwa timu nyingine kwa mkopo. Inamaana siku ya jumapili ndipo kitakapojulikana kikosi rasmi kitakachoshiriki ligi kuu msimu ujao kwani ambaye atakuwa hajaitwa maana yake safari yake itakuwa imesihia hapo ingawa tayari uongozi umeshapeleka barua na taarifa kwa wachezaji walioachwa.

COASTAL UNION
2 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA  


No comments:

Post a Comment