Sunday, July 21, 2013

Coastal Union yampa pole Razak Khalfan kwa kufiwa na baba yake.

Razak Khalfan akiwa hotel ya JB Belmont jijini Mwanza, walipoalikwa na Marehem Mzee JB baada ya kuonyesha soka la uhakika walipokutana na Toto African kwenye mechi za ligi kuu mzunguko wa pili msimu uliopita.
Razak Khalfan aliyesimama katikati akimwangalia Selembe (7) akitoa pasi kwa Danny Lyanga (3) huku mchezaji wa African Lyon akijaribu kumdhibiti Danny. Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kwenye mechi za mzunguko wa pili ligi kuu Bara msimu uliopita. Coastal Union ililala kwa bao 1-0. 


Uongozi wa Coastal Union unatoa salamu za rambirambi kwa Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Razak Khalfan kutokana na kifo cha baba yake Mzee Khalfan kilichotokea jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu kutoka jijini Tanga mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema walipata taarifa jana kuhusiana na msiba wa mzazi wa Razak na wamempa ruhusa kuhudhuria mazishi kwani tayari alisharipoti kambini.
“Ni kweli Razak amefiwa na baba yake na tayari tumeshampa ruhusa, uongozi pamoja na wanachama unasikitika sana kuhusiana na taarifa hizo. Razak Khalfan ni mwenzetu tumekuwa naye kwa amani hivyo msiba wake ni wetu, “ alisema Aurora.
Blog hii imepata taarifa kuwa mzazi wa mchezaji huyo amezikwa leo alasiri jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Mbagala kiburugwa shimo la mchanga.
Aidha kwa mujibu wa Razak, mzee wake alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi ‘stroke’ kwa kipindi kirefu lakini jana alianguka wakati akiwa msalani na kwa mujibu wa madaktari alivuja damu ndani ya ubongo na kuganda.
Sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Mbele yake nyuma yetu.
COASTAL UNION
21 JULAI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment