Tuesday, July 9, 2013

Coastal Union U20 Vs JKT Oljoro U20, Rollingstone Cup Arusha.

Kikosi cha Coastal Union U20 Kilichoanza.
Kama kawaida vijana huomba dua kumtanguliza Mungu kabla ya mechi.
Manahodha wa timu zote mbili wakipata picha ya pamoja na waamuzi wa leo.

Kikosi cha Coastal Union chini ya miaka 20 leo wanaendesha kampeni yao ya kutwaa ubingwa wa michuano ya soka kwa vijana Rollingstone Cup inayoendelea jijini Arusha kwa kutupa karata yao ya pili dhidi ya maafande wa JKT Oljoro uwanja wa  kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid alasiri hii.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Arusha kocha mkuu wa timu ndogo Bakari Shime ‘Super Coach’, amesema wamejiandaa vizuri na mashabiki wategemee mambo makubwa kwani katika kundi lao hakuna timu itakayomsumbua na hata katika kundi B ambamo kuna timu watakazokutana nazo kwenye hatua ya robo fainali pia hakuna timu ya kuwatisha.
“Kwa sasa tunajipanga kuangalia ni timu gani tutakutana nayo tukifika fainali, kwa maana makundi yote hayana timu za kutisha uzoefu wa miaka miwili kwenye michuano hii inatupa kiburi cha kucheza soka la uhakika bila papara, hivyo we subiri tu kushangilia,” alisema Shime.
Kikosi kilichoanza leo ni 1. Mansour Alawi, 2.Mwaita Saleh, 3.Hussein Amri ‘Zolla’, 4.Nzara Ndaro (captain), 5.Yusuf Chuma ‘Croach’, 6.Aziz Fatawi, 7.Mohammes Issa ‘Banka’, 8.Behewa Sembwana, 9.Mohammed Hassan, 10. Alli Nassor ‘Ufudu’, 11.Ayoub Semtawa.
Vijana  jana walicheza na Young Life wakashinda 3-0 keshokutwa watashuka dimbani kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya Testimonial Academy.
Mpira unaendelea huko Arusha tutaleta taarifa zaidi maana mpaka sasa imefikia dakika ya 30 matokeo ni 0-0. Gemu ni ngumu ya vuta nikuvute Coastal Union wameshapata kona nne wakati JKT Oljoro wamepata kona moja.
COASTAL UNION
9 Julai, 2013


No comments:

Post a Comment