Tuesday, July 2, 2013

Kikosi Coastal Union B, kitakachoshiriki Rolling Stone kuwekwa wazi wiki hii.

 Kwa mbaali kocha mkuu wa vijana chini ya miaka 20 Coastal Union, Bakari Shime (aliyeshika kitabu) akiangalia kwa makini vijana wa kuenda nao Arusha wakati wa mechi dhidiya Beach Dume. Anayeonekana hapo mbele ni mwandishi wa Coastal Union Hafidh Kido.

 Hawa ni wanachama wa tawi la Coastal Union Nyumba wakiwa nje ya klabu wakicheza keram.

Mkurugenzi wa ufundi wa coastal Union Nassor Binslum akionyesha uwezo wake wakati timu ya vijana ikipambana na Beach Dume jumamosi iliyopita katika uwanja wa Popatlal ambapo Coastal Union waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Bakari Mkumba na Emmanuel John.

Muda si mrefu kocha mkuu wa timu ya vijana chini ya miaka 20 Coastal Union, Bakari Shime atatangaza kikosi kitakachokwenda Arusha katika mashindano la Rolling Stone  yanayoandaliwa na East and Central Africa Youth Football Academies Association (ECAYFA).

Akizungumza na mwandishi wa blog hii wiki iliyopita wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya vijana ‘Beach Dume’ kutoka nje kidogo ya jiji la Tanga iliyochezwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari Popatlal, ambapo Coastal Union waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 Shime alisema inamuwia vigumu kuchagua nani na nani aende Arusha kwani wachezaji ni wengi na wote wana vipaji.

“Mpaka sasa kuna vijana 40 waliokuja kwenye majaribio na wote ni wazuri, lakini lazima tuwe na kikosi chenye wachezaji wachache watakaotuwakilisha kwenye michuano ya Rolling Stone mjini Arusha,” Shime.

Michuano hiyo ambayo natarajiwa kuanza Julai 9 na kufikia kikomo Julai 19 mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha utashirikisha timu za vijana kuanzia miaka 14 mpaka 20 kutoka mataifa yote ya ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Itakumbukwa mwaka jana Coastal Unaion walifanya vizuri kwenye michuano ya vijana yaani Rolling Stone na Uhai Cup. Kwenye Rolling Stone ya mwaka jana iliyofanyika nchini Burundi vijana walifika mpaka fainali wakatolewa kwa penati na timu kutoka jamhuri ya Congo iitwayo Ecofoot.

Meneja wa timu ndoogo Abdulrahman Mwinjuma ‘Ubinde’ amesema “Mwaka jana tulikuwa na kikosi kizuri sana niliumia tulipokuwa Burundi kwenye fainali ambapo tulitolewa kwa mikwaju ya penati na timu kutoka Congo, lakini hatukuvunjika kwani moyo mwaka huohuo tukashiriki kombe la Uhai jijini Dar es Salaam tukafika fainali tena na tukatolewa kwa mikwaju ya penati na timu ya vijana Azam FC, lakini mwaka huu tumeamua kila michuano tunatwaa ubingwa.”

Coastal union chini ya miaka 20 imeanzishwa kwa utaratibu mpya wa shirikisho la soka nchini TFF ambapo Rais wa shirikisho hilo Leodger Tenga aliamua kila timu inayotaka kushiriki ligi kuu lazima iwe na timu ya vijana chini ya miaka 20.

Mafanikio makubwa waliyowahi kupata timu B ya wagosi wa kaya ni kufika fainali mbili za michuano migumu ya Rolling Stone na Uhai Cup. Ambapo katika michuano ya Uhai Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana kocha Bakari Shime alichaguliwa kuwa kocha bora wa michuano na golikipa wa Coastal Union ambaye amepandishwa timu kubwa Mansour A. Mansour alichaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano.

COASTAL UNION
1 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA






No comments:

Post a Comment