Sunday, July 21, 2013

Morocco achekelea kikosi chake Tanga.

Kocha mkuu wa Coastal Union, Hemed Morocco akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga wiki iliyopoita.
Wachezaji wa Coastal Union wakifanya mazoezi ya umakini wa luoa na kupokea pasi na kumiliki mpira wakati wa mazoezi.
Atupele Green akinyoosha misuli katika uwanja wa Mkwakwani wakati wa mazoezi ya Coastal Union.
Kocha msaidizi wa Coastal Union, Ally Kidi akiwaangalia vijana wake wakinyoosha msuli uwanja wa Mkwakwani Tanga.



Kocha wa Coastal Union ya Tanga, Hemed Morocco amesema anafurahishwa na viwango vinavyoonyeshwa na wachezaji wake wakiwamo nyota wa Simba waliohamia klabu hiyo.
Union iliyo kambini Raskazoni, inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga ikijiandaa na Ligi Kuu msimu ujao unayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Morocco aliliambia gazeti hili jana kuwa, tangu aanze mazoezi vijana wake wameonyesha kujituma na kufanya mazoezi kwa bidii.
“Nashukuru mazoezi yanakwenda vizuri, mpaka sasa wachezaji wote wameripoti kambini, ushindani umeongezeka kama mnavyojua kutokana na kuwepo kwa wachezaji wenye uwezo,” alisema Morocco. Alisema uwepo wa wachezaji wapya ndani ya kikosi chake kumeongeza ushindani mkubwa miongoni mwa wachezaji. Baadhi ya wachezaji wapya na wenye uzoefu ni Haruna Moshi Boban, Uhuru Seleman na Juma Nyosso waliojiunga kutoka Simba na Azam FC.
CHANZO: GAZETI MWANANCHI JUMAPILI

No comments:

Post a Comment