Thursday, August 29, 2013

Coastal Union na Yanga zaingiza mil 152.

                                                         Hemed Moroco kazini jana...

Ally Mustafa ' batez' golikipa wa Yanga akijaribu kumhadaa nahodha wa Coastal Union, Jerry Santo kabla hajapiga penati ya jana. Yanga na Coastal Union walitoka suluhu ya 1-1, bao la Yanga ilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 64 kipindi cha pili baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa kutoka winga ya kushoto. Bao la Wagosi lilifungwa kwa njia ya penati dakika ya 90 baada ya Luhende wa Yanga kuushika mpira eneo la hatari.




MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 152,296,000.

Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa Sh. 5,000, Sh. 8,000, Sh. 15,000 na Sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa Sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh. 23,231,593.22.

Mgawo mwingine ni asilimia 15 ya uwanja Sh. 18,786,827.52, tiketi Sh. 3,818,890, gharama za mechi Sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi Sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh. 4,383,593.09.


Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF
29 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment