Saturday, February 9, 2013

Soma list ya wachezasji na viongozi waliopo Mwanza....

 Hamad Juma ambae amepandishwa kutoka timu B akishuka katika basi la timu mara baada ya kufika uwanja wa ndege Dar es Salaam jana alasiri.

 Hapa anaonekana Ibrahim Twaha 'Messi', philip Mugenzi, Othman Tamim, kocha Morrocco na Shengo kwa jaaam. Hapa walikuwa wanashuka uwanja wa ndege wa Mwanza.

 Messi akinyoosha misuli uwanja wa Kirumba jana jioni mara baada ya kutua kutoka ndani ya pipa. Ila huyu pipa ameshalizoea maana yupo timu ya Taifa chini ya miaka 20. Kila siku wanapaa angani.


 Sahaaban Kado na Rajabu Kaumbu wakifanya mazoezi jana katika uwanja wa Kirumba.

 Ahahahaaaa hii picha inanichekesha sana, Barbosa yu maaajiii halafu Sipi bado anaomba pasi... maana yake mpira ukija hapo Mbrazil lazima ajute.


Hapa viongozi wa msafara wakiwapa mawaidha vijana baada ya mazoezi. Waliosimama kutoka kulia Bawazir na wa pili alievaa shati la draft ni mwenyeji wetu wachezaji wanakula hotelini kwake anaitwa Seif. Huyu jamaa anaijua Coastal kuliko mtu yeyote. Alinitajia list ya mwaka 1984 mwenyewe nilikoma, Ni mtu wa Tanga pia huyu ila alihamia Bukoba tangu miaka ya thamanini. anadai ameshaipokea Coastal mara nyingi sana tangu mwaka 1988 enzi za kina Juma Mgunda, Ally Maumba, Hussein Mwakuruzo na wengine wengi. 



Kikosi cha Coastal Union ya Tanga kimeshawasili katika jiji la Mwanza tangu jana saa kumi alasiri kwa ndege ya shirika la Fistjet ambapo waliondoka jijini Dar es Salaam majira ya saa tisa na nusu na kukaa angani takriban saa moja na robo.

Baada ya kufika kambini kwa basi la kukodi timu ilijiandaa kuelekea uwanja wa Kirumba kwa ajili ya mazoezi mepesi ya kuondoa uchovu na kunyoosha misuli.

Coastal Union inacheza mchezo wao wa tatu wa ligi kuu bara mzunguko wa pili na Toto Africa inayofuliwa na John Tegete yenye makazi jijini humo, ambapo timu ya wagosi wa kaya itaendelea kuwepo katika kanda ya ziwa mpaka tarehe 14 watakaporejea kwa usafiri huohuo wa anga kurudi jijini Dar es Salaam na baadae Tanga mara baada ya kucheza na Kagera Sugar ya Bukoba.

Timu itaondoka siku ya jumatatu asubuhi kuelekea Bukoba kwa usafiri wa basi kukabiliana na Kagera Sugar inayonolewa na King Abdallah Kibaden mnamo tarehe 13 mwezi huu, ambapo wagosi wa kaya wanashuka dimbani kucheza mechi hizo mbili za kanda ya ziwa zikiwa na point 26 kibindoni maana yake wakishinda mechi zote mbili watajihakikishia kupanda nafasi moja juu yaani nafasi ya tatu inayoshikiliwa na wekundu wa msimbazi Simba.


Wachezaji walioandamana na timu ni ishirini ambao ni Shaaban Kado, Rajabu Kaumbu, Ismail Suma, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Mbwana Hamis ‘Kibacha’, Castro Mumbala, Joseph Mahundi, Mohammed Sudi, Gerrald lukindo, Ibrahim Hussein ‘Messi’, Gabriel Barbosa, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Danny Lyanga, Jerry Santo, Hamad Juma, Nzara Ndaro, Hamis Shengo, Abdi Banda, Razak Khalfan.

Viongozi waliokuwemo katika msafara huo ni Mwenyekiti Hemed Hilal ‘Aurora’, Bawazir, meneja Akida Machai, Mzee ali, daktari wa timu Mzee Kitambi Mganga, makocha wapo watatu ambao ni kocha mkuu Hemed Morroco, kocha saidizi Ally Kidi na kocha walinda mlango Juma Pondamali ‘Mensah’.

Kila la heri leo katika uwanja wa CCM Kirumba saa kumi alasiri timu inatoa salamu kwa wakazi wa Tanga kuwa heshima ya soka katika mji huo itarudi kwa nama yoyote ile. Coastal tweendeee…

COASTAL UNION
9 Feb, 2013
Mwanza, Tanzania

No comments:

Post a Comment