Saturday, February 9, 2013

Soma tathmini mchezo wa jana Toto African 0-0 Coastal Union

Ibrahi Twaha akimsaidia Danny Lyanga kuelekea kwenye vyumba vya kubadili nguo baada ya mechi, Danny aliumizwa paja wakati wa mchezo.



                                                The beautiful view of Mwanza, lake zone.

Timu ya Coastal union jana ilishuka dimbani kucheza mchezo wao wa tatu wa ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili dhidi ya Toto Africa ya jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mpaka mwamuzi kutoka Morogoro anapuliza kipenga cha mwisho kuashiria mechi imekwisha hakukuwa na mbabe kwa timu zote mbili yaani matokeo yalikuwa ni suluhu ya bila kufungana.

Wagosi wa kaya watajilaumu sana kwa kushindwa kupata point tatu muhimu ambazo zingewawezesha kupanda nafasi moja juu, lakini bahati haikuwa yao baada ya kuambulia suluhu ambayo inawafanya wawe na point 27 zinazowafanya waendelee kungangania nafasi ya nne chini ya wekundu wa msimbazi Simba waliosuluhu na JKT Oljoro mjini Arusha jana ambao wana point 29. Kwani nafasi ya kwanza inashikiliwa na Yanga wenye point 33 ya pili ikishikiliwa na Azam FC wenye point 30.

Siku ya jumatano tarehe 13 mwezi huu wagosi wa kaya watakamilisha ziara yao ya kanda ya ziwa kwa kucheza na Kagera sugar kwenye uwanja wa kaitaba huku wakiwa na tahadhari kubwa kwani kwa mchezo wa jana tu wachezaji wanne wa Coastal Union walipewa kadi za njano akiwemo golikipa Shaaban Kado, wakati Kagera wanashuka dimbani na wagosi wakiwa na point 24 mkononi sawa na Ruvu Shooting ambao wote wanaimezea mate nafasi ya nne katika msimamo.

Jana kulichezwa mechi nne katika viwanja tofauti ambapo uwanja wa Kaitaba Bukoba Kagera Sugar walitoka suluhu ya 1-1 na Mgambo JKT, wakati JKT Oljoro waliinyima point za bwerere Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kwa kutoka suluhu ya 1-1, wajelajela Tanzania Prison waliichabanga 2-0 Africa lyon, na kuondoa sherehe ya sare katika mechi zote nne za ligi kuu baada ya Coastal Union kutoka suluhu ya 0-0 na Toto Africa uwanja wa CCM Kirumba.

Kikosi cha jana cha Coastal Union kilichokutana na Toto africa ni: 

1.Shaban Kado
2.Ismail Suma
3.Othaman Tamim
4.Philipo Mugenzi
5.Mbwana Khamis(Kibach)
6.Jerry Santo
7.Joseph Mahundi
8.Razak Khalfan
9.Daniel Lyanga
10.Mohamed Sudi
11.Seleiman Kassim(Salembe)

Sub
1.Rajab Kaumbu
2.Gerald Lukindo
3.Ibrahim Twaha
4.Gabriel Barbosa
5.Hamad Juma
6.Khamis Shengo
7.Abdi Banda



Ambapo baadae mwalimu alifanya mabadiliko dakika ya 75 kwa kumtoa Danny Lyanga na kumuingiza Gabriel Barbosa, mnamo dakika ya 77 alitoka Othman Tamim akaingia Abdi Banda na baadae akatoka Mahundi akaingia Ibrahim Twaha.
  

 

 Leo Mtibwa Sugar watashuka dimbani na wauza Ice Cream Azam FC katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro ambapo matokeo mazuri yatasababisha Azam kufanana point na vinara wa ligi Yanga wakati Mtibwa Sugar wakishinda kutawafanya kufanana point na wagosi wa kaya.

Kwa faida ya wapenzi wa timu yetu huo ndiwo msimamo wa ligi baada ya mechi za jana tarehe 9 Feb.

Pos. Club P W D L GF GA GD Pts
1 Young Africans SC 15 10 3 2 28 12 16 33
2 Azam FC 15 9 3 3 23 13 10 30
3 Simba SC 16 7 7 2 25 14 11 28
4 Coastal Union SC 16 7 6 3 19 15 4 27
5 Ruvu Shooting Stars JKT 15 7 3 5 20 17 3 24
6 Kagera Sugar FC 16 6 6 4 17 15 2 24
7 Mtibwa Sugar FC 15 6 5 4 19 14 5 23
8 JKT Oljoro FC 16 5 6 5 19 18 1 21
9 Tanzania Prisons 15 4 6 5 10 12 -2 18
10 JKT Mgambo 16 5 3 8 11 16 -5 18
11 JKT Ruvu Stars 15 4 4 7 14 22 -8 16
12 Toto African 17 2 7 8 13 24 -11 13
13 Polisi Moro 15 2 4 9 6 16 -10 10
14 African Lyon FC 16 2 3 11 10 26 -16 9

Coastal Union
10,02,2013
Mwanza, Tanzania

No comments:

Post a Comment