Wednesday, July 3, 2013

Angalia mazoezi ya timu ndogo wakijiandaa na Rolling Stone.



Kocha wa walinda mlango Juma Pondamali 'Mensah' akiwafua vijana wake.


Golikipa namba tatu wa Coastal Union kubwa Mansour A Mansour, akiwa kazini mwenyewe ameomba kuichezea timu ya vijana kwa mapenzi tu, na kocha hajamkatalia.
Mchezaji wa Coastal Union B 'mwenye rasta' akichuana na mchezaji wa Beach Dume siku ya jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Popatlal. Huyu kijana sikulipata jina lake lakini nimesikia wenzake wakimuita Kiemba.

Ally Albusaid naye alikuwepo.

Kutoka kushoto mwenyekiti wa hamasa, Miraji Wandi 'Shoka', wa pili aliyekaa Meneja wa timu B Abdulrahman Mwinjuma 'Ubinde' aliyesimama mwenye kanzu ni meneja msaidizi timu B bwana Seif na aliyekaa ni msimamizi wa matokeo kwenye ukurasa wa timu Ally Albusaid, wakifuatilia mazoezi ya vijana katika uwanja wa sekondari Popatlal mjini Tanga.
Kocha mkuu wa timu B, Bakari Shime akiangalia vijana wake wakijifua.
Shime akihakikisha jina la kijana wa timu B wakati wa mazoezi wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment