Kikosi cha Coastal Union U20 Kilichoanza. |
Kama kawaida vijana huomba dua kumtanguliza Mungu kabla ya mechi. |
Manahodha wa timu zote mbili wakipata picha ya pamoja na waamuzi wa leo. |
Kikosi cha Coastal Union chini ya miaka 20 leo wanaendesha
kampeni yao ya kutwaa ubingwa wa michuano ya soka kwa vijana Rollingstone Cup
inayoendelea jijini Arusha kwa kutupa karata yao ya pili dhidi ya maafande wa
JKT Oljoro uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh
Amri Abeid alasiri hii.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Arusha kocha mkuu wa
timu ndogo Bakari Shime ‘Super Coach’, amesema wamejiandaa vizuri na mashabiki
wategemee mambo makubwa kwani katika kundi lao hakuna timu itakayomsumbua na
hata katika kundi B ambamo kuna timu watakazokutana nazo kwenye hatua ya robo
fainali pia hakuna timu ya kuwatisha.
“Kwa sasa tunajipanga kuangalia ni timu gani tutakutana nayo
tukifika fainali, kwa maana makundi yote hayana timu za kutisha uzoefu wa miaka
miwili kwenye michuano hii inatupa kiburi cha kucheza soka la uhakika bila
papara, hivyo we subiri tu kushangilia,” alisema Shime.
Kikosi kilichoanza leo ni 1. Mansour Alawi, 2.Mwaita Saleh,
3.Hussein Amri ‘Zolla’, 4.Nzara Ndaro (captain), 5.Yusuf Chuma ‘Croach’, 6.Aziz
Fatawi, 7.Mohammes Issa ‘Banka’, 8.Behewa Sembwana, 9.Mohammed Hassan, 10. Alli
Nassor ‘Ufudu’, 11.Ayoub Semtawa.
Vijana jana walicheza
na Young Life wakashinda 3-0 keshokutwa watashuka dimbani kukamilisha hatua ya
makundi dhidi ya Testimonial Academy.
Mpira unaendelea huko Arusha tutaleta taarifa zaidi maana
mpaka sasa imefikia dakika ya 30 matokeo ni 0-0. Gemu ni ngumu ya vuta nikuvute
Coastal Union wameshapata kona nne wakati JKT Oljoro wamepata kona moja.
COASTAL UNION
9 Julai, 2013
No comments:
Post a Comment