Hapa anajadiliana na meneja Ubinde kuwa ni vema wakaondoka mapema ili kufika kabla muda wa futari.
Jambo likakubalika na hapo safari ikaanza kutengenezwa.
Vijana wakiwa nje kusubiri suala fulani likamilike safari ianze kuelekea mjini, dereva alishauri kuondoka mapema ila kutokana na mambo kuenda kombo ikabidi waondoke mchana.
William akiwa na vijana wake wanapiga story wakati wanasubiri mipango ya kuondoka ikamilike. picha ya juu ni Hamad Juma 'Basmat' na picha ya chini ni team captain Nzara Ndaro Nzara.
Hapa vijana walishuka kuchimba dawa ilikuwa saa kumi alasiri maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro.
Tulipofika wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro tukanunua bidhaa iwe zawadi mkono mtupu haurambwi atii.
Wamasai nawo wakataka kutuuzia ugoro, ati kisa wamesikia tunatoka Tanga. |
Tanzania inapendeza kutokana na kuwa na mbuga nyingi za wanyama, hii ni miongoni mwa mbuga ndogo za wanyama ipo Mkoa wa Kilimanjaro wilayani Same. Ni Mkomazi National Park.
Meneja akiwaonyesha vijana wake mahala watakapokaa, hii ni kambi mpya ya Coastal Union Raskazone Hotel..
Basi na admin hata picha moja nisionekane?
COASTAL UNION
17 Julai, 2013
TANGA, TANZANIA
No comments:
Post a Comment