Wednesday, July 3, 2013

Nimebaini watu wa Tanga wanaipenda sana timu B.

 Hapa meneja Ubinde akifuatilia mazoezi ya walinda mlango wake katika uwanja wa Popatlal jumamosi.

Yusuf Chuma 'Croch' mwenye jezi nyekundu akihakikisha ndugu zake wanafanya vizuri kwenye mazoezi. Huyu kijana namkubali sana licha ya kupandishwa timu kubwa kwa mkataba mnono na mshahara wa uhakika lakini ameamua kujitolea kushiriki Rolling stone kwasababu umri unamruhusu na ana mapenzi na klabu yake.
Jembe langu Thabeet 'mwenye fulana ya Tusker' akikokota mpira wakati wa mazoezi.

 Taraa huyu ndo huyo muhindi anayeupiga mwingi kama ulisikia taarifa zake, huko Arusha patakuwa hapatoshi jamani.

Meneja Ubinde na kocha Shime wakibadilishana mawili matatu.
Mwenyekiti Aurora , wmenye fulana nyekundu akiwa na wazee wa Coastal Union kwenye mazoezi ya vijana.
 Shime akiangalia vijana wake wakipasha viungo kabla ya kuumana na Beach Boy timu ya vijana kutoka nje kidogo ya mji wa Tanga katika mechi ya kujipima nguvu. Coastal Union walishinda 2-1.

                      Kutoka kushoto Shime, Binslum na Ubinde wakiangalia ufundi wa timu ya vijana.

Laiti ningekuwa na uwezo ningemshauri mwalimu Shime asimuache huyu Kiemba, maana ana nguvu na anajua kumiliki mpira.
 Aaaaaaaa Ufudu weeeee, huyu kijana ana mbio, akili na nguvu. Mungu atupe nini sisi Coastal Union timu zote tamu ya wakubwa na wadogo.

 Hili bao tulilikosa kiajabu sana maana Kiemba alipiga mpira kama anaogelea, ahahaa lakini kukosea pia kumo.

Wakinamama waliokuja na Beach Boy kushangilia walitaka kuanzisha balaa baada ya kuambiwa madera yao yana nongo... Chezeya Shoka na Unenge wewe?

.....picha zinaendele...

No comments:

Post a Comment