Hawa ni wanachama wa tawi la Coastal Union Nyumba wakiwa nje ya klabu wakicheza keram.
Muda si mrefu kocha mkuu wa timu ya
vijana chini ya miaka 20 Coastal Union, Bakari Shime atatangaza kikosi
kitakachokwenda Arusha katika mashindano la Rolling Stone yanayoandaliwa na East and Central Africa
Youth Football Academies Association (ECAYFA).
Akizungumza na mwandishi wa blog
hii wiki iliyopita wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya vijana ‘Beach
Dume’ kutoka nje kidogo ya jiji la Tanga iliyochezwa kwenye uwanja wa shule ya
sekondari Popatlal, ambapo Coastal Union waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 Shime
alisema inamuwia vigumu kuchagua nani na nani aende Arusha kwani wachezaji ni
wengi na wote wana vipaji.
“Mpaka sasa kuna vijana 40
waliokuja kwenye majaribio na wote ni wazuri, lakini lazima tuwe na kikosi
chenye wachezaji wachache watakaotuwakilisha kwenye michuano ya Rolling Stone
mjini Arusha,” Shime.
Michuano hiyo ambayo natarajiwa kuanza
Julai 9 na kufikia kikomo Julai 19 mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh
Amri Abeid jijini Arusha utashirikisha timu za vijana kuanzia miaka 14 mpaka 20
kutoka mataifa yote ya ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Itakumbukwa mwaka jana Coastal
Unaion walifanya vizuri kwenye michuano ya vijana yaani Rolling Stone na Uhai
Cup. Kwenye Rolling Stone ya mwaka jana iliyofanyika nchini Burundi vijana
walifika mpaka fainali wakatolewa kwa penati na timu kutoka jamhuri ya Congo
iitwayo Ecofoot.
Meneja wa timu ndoogo Abdulrahman Mwinjuma
‘Ubinde’ amesema “Mwaka jana tulikuwa na kikosi kizuri sana niliumia tulipokuwa
Burundi kwenye fainali ambapo tulitolewa kwa mikwaju ya penati na timu kutoka
Congo, lakini hatukuvunjika kwani moyo mwaka huohuo tukashiriki kombe la Uhai
jijini Dar es Salaam tukafika fainali tena na tukatolewa kwa mikwaju ya penati
na timu ya vijana Azam FC, lakini mwaka huu tumeamua kila michuano tunatwaa ubingwa.”
Coastal union chini ya miaka 20
imeanzishwa kwa utaratibu mpya wa shirikisho la soka nchini TFF ambapo Rais wa
shirikisho hilo Leodger Tenga aliamua kila timu inayotaka kushiriki ligi kuu
lazima iwe na timu ya vijana chini ya miaka 20.
Mafanikio makubwa waliyowahi kupata
timu B ya wagosi wa kaya ni kufika fainali mbili za michuano migumu ya Rolling
Stone na Uhai Cup. Ambapo katika michuano ya Uhai Cup yaliyofanyika mwishoni
mwa mwaka jana kocha Bakari Shime alichaguliwa kuwa kocha bora wa michuano na
golikipa wa Coastal Union ambaye amepandishwa timu kubwa Mansour A. Mansour
alichaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano.
COASTAL UNION
1 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment