Sunday, July 7, 2013

Historia iliyotukuka Tanga.



Historia inasema hapa ni uwanja wa Taifa ‘shamba la bibi’ katika mechi kati ya Coastal Union na Young Africans.

Kutoka kushoto ni Mzee mrisho "mbunge", Salim Mazrui, daktari wa timu Francis Mganga, Ali Jangalu, Majisu, na Mohammed Mwameja. Mstari wa kati;  Rifat Said, Razak Yusuf ‘Careca’, Ali Majeshi, Raphael John, Mohammed Kampira ‘ka-ball’, Deoniz John, Salim Mohamed.
Murjan Mwinyi (mtoto), Kingsley, Douglas Muhani, kolongo, Reuben Mgaza, Mdoe, Hussein Mwakuluzo na Ali kiraka (mtoto).
Aidha kwa maelezo ya Hussein Mwakuluzo katika mwaka huo Abuu Yassin Napili na Juma Mgunda walikwenda nchini Oman kucheza soka ndipo wakasajiliwa Kingsley Marwilo kutoka RTC Shinyanga, Deoniz John kutoka RTC Mwanza na Reuben Mganza kutoka Akiba ya Pwani kuziba mapengo ya kina Mgunda.
Kadhalika Salim ‘Mkuwait’ alitoka timu ya vijana Ilala Dar es Salaam alikuwa fundi sana wa mpira anauchezea anavyotaka yeye, katika mechi za Afrika mahsriki na kati alifunga mabao 2 peke yake kwa vichwa timu ya Small Simba katika uwanja wa nyumbani Mkwakwani.
Katika kumbukumbu nyingine ya kikosi hiki ni mchezaji Rafael John ambaye alitoka timu hasimu ya African Sports ya barabara 12 kuziba pengo la Ali Maumba ambaye aliondoka kikosini.
Je Coastal Union ya miaka hiyo itaweza kurudi kutokana na usajili wa nguvu uliofanywa mwaka huu?
COASTAL UNION
7 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment