Uongozi wa Coastal Union unatoa taarifa rasmi kuwa wachezaji
wote wanatakiwa kuripoti kambini siku ya jumapili Julai 7 mwaka huu kwa ajili
ya kuanza mazoezi kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi Nassor Binslum ambaye
ndiye ana mamlaka ya kusimamia masuala yote yanayohusu mazoezi na mikakati ya
ushindi dimbani, amesema wachezaji wameshaanza kupewa taarifa juu ya kuanza
mazoezi mapema mwezi huu.
“Viongozi wamekaa na wamekubali mazoezi yaanze tarehe 7
mwezi huu, kwa sasa kambi yetu ambayo ni Raskazone Hotel ipo katika matengenezo
mpaka itakapofika tarehe saba kila kitu kitakuwa tayari kuanzia wapishi,
vitanda na magodoro pamoja na walinzi wa kambi, hivyo ieleweke tu kuwa mazoezi
yanaanza mwishoni mwa wiki hii,” alisema Binslum.
Hata hivyo uongozi mbali ya kusajili wachezaji wapya bado
haijaweka wazi juu ya wachezaji wa zamani walioacha na waliopelekwa timu
nyingine kwa mkopo. Inamaana siku ya jumapili ndipo kitakapojulikana kikosi
rasmi kitakachoshiriki ligi kuu msimu ujao kwani ambaye atakuwa hajaitwa maana
yake safari yake itakuwa imesihia hapo ingawa tayari uongozi umeshapeleka barua
na taarifa kwa wachezaji walioachwa.
COASTAL UNION
2 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment