Wednesday, July 3, 2013

Bakari Shime.....Mashine ya kutengeneza vijana wa kuikomboa Coastal Union.




Anaitwa Bakari Shime, ndiye kocha mkuu wa timu B, ameleta mapinduzi makubwa sana katika soka la vijana jijini Tanga. Mpaka kufikia kutunukiwa tuzo ya kocha bora wa timu za vijana mwaka jana.

Amefanikiwa kuifikisha Coastal Union B fainali mbili katika michuano inayoheshimika Afrika Mashariki na kati.

Alipata kucheza Jazinho FC ya Tanga na kufundisha Cabo Delgado na Eagle FC zote za vijana, ameleta mchango mkubwa sana maana katika vijana sita waliopandishwa timu ya wakubwa wote wamepitia mkononi mwake, yaani amewalea mwenyewe.

Imetolewa hoja wanazi wa Wagosi wa Kaya kuwa uongozi wa klabu umfikirie kumtafutia chuo cha kuongeza ujuzi wa kufundisha ili awe kocha mkali zaidi kwa vijana hasa ikizingatiwa Coastal Union inafikiria kuanzisha Academy ya soka la vijana.

Nadhani hilo litapewa uzito na uongozi wetu makini na sikivu. Muda si mrefu tutaleta historia yake kamili kuanzia shule aliyosoma mpaka hapa alipo.

COASTAL UNION
3 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA



No comments:

Post a Comment