Wednesday, July 17, 2013

Mazoezi yamepamba moto na mashabiki hawapo nyuma....

Othman Tamim akionyesha uwezo wake wa kucheza na mpira wakati wa mazoezi uwanja wa Mkwakwani jana.

Mohammed Miraji na Kibacha huyu aliyevaa na mba 19 ni Abdi Banda lakini huyu wa kushoto sijapata jina lake.

Kumbe Shaaban Kado naye anaupiga mwingi kweli akicheza ndani, hapa anatafuta mbinu za kumtoka beki wake Philip Mugenzi.

Mohammed Sudi akirudisha mpira kwa Atupele, mazoezi haya yanamjenga mchezaji kutoa pasi za uhakika.

Raha ya jukwaa hili kuna vigogo watupu na ubishani wa kuijua Coastal Union ndipo mahala pake.

Kwa mbele kabisa (mwenye kalamu mfukoni) namuona mzee wa gubu almaaruf Unenge. Kawaida hapendi kuchezewa hasa linapokuja suala la maslahi ya Coastal Union.

El Siagi mzuka wa ubishani umemkolea hapa.
                Mwalimu Morocco akipanga vifaa vyake vya kazi ili kuhakikisha wachezaji wanajifua hasa.

                                           Ally 'Kidi' akitoa mbinu kwa wachezaji wake.

Uhuru Suleiman amekuwa mwepesi sana hakika mwaka huu timu imekamilika, sikutegemea kumuona vile baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu. Hatuna cha kujutia kwa usajili huu.

COASTAL UNION
17 JULAI,2013
TANGA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment