Timu B ya Coastal Union itashuka dimbani kesho kutupa karata
yao ya mwanzo dhidi ya Young Life ya mjini Arusha kwenye michuano maarufu ya
vijana wanaotoka nchi za Afrika Mashariki na kati, Rolling Stone.
Michuano hiyo inayofanyika jijini Arusha imeanza rasmi jana
ambapo Azam FC waliibuka na karamu ya mabao 3-0 dhidi ya Eagle FC kutoka Tanga
hivyo kuwa mwanzo mbaya kwa mkoa wa Tanga.
Kwa mujibu wa meneja wa timu B, Abdulrahman Ubinde timu
imewasili jana jioni ikiwa na wachezaji 20, kocha Bakari Shime pamoja na
daktari wa timu Mzee Francis Mganga, tayari kuanza kampeni ya kuchukua ubingwa.
Mpaka sasa ratiba rasmi ya michuano hiyo haijatolewa kwani
zipo taarifa kuwa baadhi ya timu zilizothibitisha ushiriki bado hazijawasili
kambini hivyo kuwawia vigumu waandaaji wa michuano hiyo kupanga ratiba kwa
kuchelea kuweka timu ambayo haitafika.
Taarifa rasmi zinaweka wazi kuwa Coastal Union watashuka
dimbani kukabiliana na Young Life kesho saa nane mchana katika uwanja wa
General Tyre jijini humo.
Mungu ibariki Coastal Union Mungu ubariki jiji la Tanga.
COASTAL UNION
7 Julai, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment