Wednesday, July 3, 2013

Hizi ni picha za mkutano mkuu uliofanyika jumapili. Kunradh picha zimetoka vibaya kwasababu ya mwanga mkali wa jua na kuta za klabu zimepakwa rangi ya mafuta zinaakisi mwanga.

 Meza kuu hii ikitafakari majibu watakayowapa wanachama walioanza kuuliza maswali magumu.

Inapobidi Katibu na mjumbe kuijadili katiba ili watoe majibu muafaka hakukuwa na budi kufanya hivyo.
Mitambo miwili hii, Wazir Top na Wandi Shoka wakitafakari kikao.

                      Ukitaka kuelewa sikiliza kwa makini hapo namuona Chuse, Kido na Oscar Asenga.

Maelezo ya kina yalihitajika sana kutuliza mizuka ya wajumbe.

Wajumbe walikuwa makini sana hawataki mchezo.
 Huyu bibi ndiye alikuwa mjumbe wa jinsia tofauti pekee wote walikuwa wanaume mwanamke alikuwa yeye tu.

 Huyu mzee Boflila ana historia kubwa sana na timu hawa ndiwo waliokunywa maji ya bendera.
 Wajumbe wenye akili walikuwa wanajenga hoja kwa kutumia vifungu vya katiba yaani hakuna longolongo.

 Shoka naye alikuwa amechamkwa kichwa kimemvuruga, halafu kuna mtu alikosa adabu akawa anazungumza hovyohovyo, shoka akasema jamani eenhh mimi nikiongea halafu mtu akiongea naona kama ananidharau ujue.... ahahaaaaa.
 Umakini ulikuwa wa hali ya juu, kwa mbaali namuona Akida Machai team manager akifuatilia kwa makini huku amewekewa ulinzi mkali na ndugu yake Abuu Machai asije akaharibu hali ya hewa. Ahahaaaa.
Wazir Top super admin wa Coastal Supporters akichangia hoja kwa hisa kali huku akitumia vifungu vya katiba.

No comments:

Post a Comment