Monday, July 15, 2013

Coastal Union njia panda mshindi wa tatu Rollingstone.

Habari zilizokuwepo sasa ni ima Coastal Union washiriki kumtafuta mshindi wa tatu dhidi ya JKT Oljoro ama la.

Leo asubuhi saa tano meneja wa timu Abdulrahman Ubinde, Kocha Bakari Shime na mwandishi wa Coastal Union Hafidh Kido walikuwa katika kikao kujadili mbali na masuala mengine lakini mustakabali wa timu kushiriki mechi ya kutafuta mshindi wa tatu baada ya fainali kuahirishwa badala ya Julai 15 na kuwa Julai 16.

Kwa mujibu wa waandaaji wa michuano hiyo baada ya kutokea vurugu jana wamiliki wa uwanja wa General Tyre palipoandaliwa kuchezwa fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, wamekataa kuendelea kutumika kwa uwanja wao kuchezewa michuano ya Rollingstone kwa madai wamekwenda kinyume na makubaliano kuwa hakutatokea vurugu na uvunjifu wa amani.

Kwa kuwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid walishazuiwa kuendelea kuutumia kwa sababu zisizojulikana hivyo ikabidi kuanzia jana waanze taratibu za kuuomba tena hivyo ikawapasa kubadili tarehe ya fainali na mshindi wa tatu.

Eagle Rangers na Coastal Union zote kutoka Tanga awali ziligomea kusogezwa mbele fainali na mshindi wa tatu kwa madai hawana fedha za kuendelea kuishi Arusha.

Eagle Rangers ambao wametinga fainali baada ya kuwachapa JKT Oljoro 2-1 waligoma kushiriki mechi ya fainali dhidi ya Azam FC waliowatoa Coastal Union katika nusu fainali kwa mikwaju ya penati 4-5.

Lakini kwa busara ya viongozi wa Rollingstone waliamua kuwachangia fedha za kujikimu Eagle Rangers, na viongozi wa Coastal Union hata walipopigiwa simu kutaka kutoa ufafanuzi juu ya ushiriki wao waliendelea kusisita kuwa hawatoshiriki mechi hiyo na wameshatoa maagizo timu irudi Tanga kesho asubuhi.

Aidha masuala ya vurugu za jana yamemalizwa kistaarabu kwa viongozi wa Rollingstone kuwataka Azam FC na Coastal Union kuzungumza na tayari mazungumzo yameshafanywa viongozi wamesameheana kilichobaki ni kulipa gharama za kioo cha gari la Azam kilichovunjwa na mtu asiyejulikana katika vurugu hizo.

kocha wa Coastal Union anasema watarejea Tanga kujipanga upya kwa ajili ya kombe la Uhai mwishoni mwa mwaka huu jijini Dar es Salaam.

COASTAL UNION
15 JULAI, 2013
ARUSHA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment